Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wahofiwa kupoteza maisha ajali ya lori, Coaster Mbeya

Ajali Mbeya Coastee Na Lori Wahofiwa kupoteza maisha ajali ya lori, Coaster Mbeya

Wed, 5 Jun 2024 Chanzo: Mwananchi

Watu ambao idadi yao haijajulikana kwa haraka wanahofiwa kupoteza maisha, kufuatia ajali iliyotokea leo Juni 5,2024 katika mteremko wa Iwambi maeneo ya Mbembela jijini Mbeya.

Habari ambazo hazijathibitishwa na mamlaka, zinaeleza kuwa lori moja lililokuwa likishuka katika mteremko huo, lililiparamia basi dogo aina ya Coaster lenye linalofanya kazi Mbeya-Tunduma na kusababisha ajali hiyo.

Mwananchi Digital iliyopo eneo hilo limeshuhudia askari polisi, wakiwamo FFU na Zimamoto wakiendelea na shughuli ya uokoaji na kuifunga barabara kwa muda.

Chanzo: Mwananchi