Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wahofia kuondolewa kwenye maeneo ya kufanyia biashara

69226 MAKONDA+PIC

Thu, 1 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Usafi wa mazingira ya mji ni jambo linaloangaliwa sana katika kipindi hiki ambacho mkutano mkuu  wa Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) wa 39 unakaribia kufanyika Jijini Dar es Salaam, Tanzania, hasa katika mitaa ya Posta. 

Mbali na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuwataka wakazi wa mkoa huo kuwa nadhifu katika kipindi chote cha mkutano, lakini wafanyabiashara ndogondogo waliopo karibu na ukumbi utakaofanyika mkutano huo nao wameanza kuonyesha mashaka ya kuondolewa katika maeneo hayo.

Ratiba ya mkutano huo inatarajiwa kuanza rasmi Agosti 5 hadi 18 mwaka huu kwa kuanza na maonyesho ya biashara na kisha mkutano mkuu wa 39 wa Wakuu wa nchi 16 za SADC, utafanyika Agosti 17 na 18, 2019.

Jana Jumatano Julai 31, 2019, Mwananchi lilifika katika eneo jirani na ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere utakaotumika kwa mkutano huo na kushuhudia wafanyabiashara mbalimbali wakiendelea na shughuli zao za kujiingizia kipato kando mwa barabara ambao baadhi walisema huenda wakaondolewa muda wowote katika eneo hilo.

 “Tumesikia tutaondolewa hapa kwa muda, lakini kutaathiri biashara zetu kwa sababu hiki kijiwe wateja wetu ni wale wanaofanya kazi ndani ya jengo hili la Diamond Plaza na wanafunzi wa Chuo cha usimamizi wa Fedha (IFM),” alisema Mickdad Seleman ambaye ni dereva wa pikipiki maarufu bodaboda katika eneo la Posta.

 Selemani alisema suala hilo liliwahi kutokea kipindi Rais mstaafu wa Marekani akiwa madarakani, Barack Obama alipotembelea Tanzania, wafanyabiashara wote wa mjini waliondolewa ili kuboresha usafi na matokeo yake, uchumi wa familia nyingi uliathirika.

Pia Soma

 Mfanyabiashara mwingine, Jumanne Mohammed ambaye ni muuzaji wa vinywaji baridi katika eneo hilo, alisema mara nyingi wanaoondolewa ni wale waliopo karibu na Ubalozi wa India na barabara ya kuelekea Hoteli ya Southern sun.

 “Yaani hao wanajua kabisa kuwa kukiwa na mkutano mkubwa wa kimataifa wao wanatafuta sehemu ya kufanyia biashara kwa muda na baadaye wanarudi au wanapumzika kabisa sisi huku hatuguswi,” alisema Mohammed.

Mama lishe, Pili Mohammed alisema wako tayari kuondolewa kwa muda katika eneo hili lakini si kuambiwa waondoke jumla kwa sababu ndiyo eneo wanalopatia kipato cha kutunza familia zao.

“Siyo mbaya kwa sababu ni dharula lakini kama hatutaruhusiwa kukaa hata sehemu nyingine huku mjini tutakufa njaa, sababu mimi ni mjane na ninalea watoto wanne wote wanategemea pesa kutoka hapa,” alisema pili.

Chanzo: mwananchi.co.tz