Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wahitimu waombwa kukumbuka walikopitia

66826 Tambaza+pic

Mon, 15 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wahitimu katika shule mbalimbali wametakiwa kukumbuka walikosoma ili kujenga hamasa kwa wanafunzi wanaoendelea na masomo, hali itakayosaidia kujua changamoto zinazokabili shule zao na kuzitatua.

Hayo yamesemwa Jumaosi Julai 13, 2019 na mwalimu wa taaluma Sekondari ya Tambaza, Simon Lupogo akipokea kompyuta mbili kutoka kwa Tambaza Alumni 1993.

Lupogo amesema wahitimu hao walichofanya ni kitu kikubwa kwa sababu Tambaza wamepita watu wengi lakini hawafanyi hivyo.

“Kompyuta mbili hizi mlizotupa zitasaidia shughuli za taasisi ya Tambaza ambayo ni endelevu. Your at (umekuwa) Tambaza siyo kwamba unapita tu itakuwa ya kwako milele,” amesema mwalimu Lupogo.

Makabidhiano hayo yameenda sambamba na tamasha kwa kutoa mada mbalimbali ikiwamo ya lishe iliyotolewa na daktari bingwa wa Saratani kutoka Hospitali ya Ocean Road, Dk Emmanuel Lugina na kuwatuza waliofanikiwa katika nyanja mbalimbali.

Lupogo amesema mtu shule hiyo ni taasisi kubwa anayepitia shuleni hapo, asiposoma mtoto wake atapita mtoto wa rafiki yake ama ndugu au mjukuu, hivyo ni shule ya Tanzania na walichokifanya wamewafanyia Watanzania.

Pia Soma

“Muwe mabalozi kwa waliopo nje hawajawahi kurudi shuleni kwao tangu wamalize, ili ilete changamoto kwa hao na wao warudi nyumbani, suala la elimu siyo la mtu mmoja kwa hiyo ni jukumu aliyepita Tambaza aweze kukumbuka kwa chochote kitu kusaidia shule yake,” amesema.

Mwalimu Lupogo alisema wakijiunga pamoja wanaweza kufanya kitu kikubwa na kwamba, hivi sasa shule hiyo inakabiliwa na upungufu mkubwa wa nyumba za walimu na mabweni.

“Utakuta watoto wanaishi magetoni kwa hiyo hili kwa sisi wana Tambaza kuanzia waliotoka miaka ya 1960 hadi 2019 tunaweza kuanza kufanya vitu kidogo kidogo, halafu tunaji-organize tukafanya fund raising tukapata fedha kidogo ya kuanza ujenzi wa bweni na watoto wakakaa pale wakafanya vizuri zaidi,” amesema.

Pia, Lupogo amewataka wahitumu hao kutenga muda wao mara kwa mara kwenda kuzungumza na wanafunzi ili kuwatia moyo na itawafundisha wakifanikiwa katika maisha yao wasisahau shule yao. 

Hata hivyo, ombi hilo limetekelezwa leo Jumatatu Julai 15, 2019 na mwenyekiti wa Tambaza Alumni 93, wakili Hussein Kitta amezungumza na wanafunzi na kuwatia moyo na kwamba uamuzi wa wao wafike wapi wanao wenyewe.

Wakili Kitta amewataka wanafunzi hao kutojali hali ya maisha kwa familia wanazotoka, kwani elimu haijali umaskini wala utajiri iwapo mtu akiamua kwa dhati kufika anakohitaji.

Katika mada yake ya lishe, Dk Lugina ambaye pia ni miongoni mwa wahitimu hao, amewataka kuepuka vyakula vya mafuta kabisa kwa sababu ni chanzo kikubwa cha shinikizo la damu mwilini na hata saratani.

“Iwapo inabidi tutumie mafuta basi tutumie yanayotokama na mimea mfano alizeti na pamba,” amesema.

Pia, Dk Lugina amesema vyakula vya wanga viliwe kwa kiasi kwani  ni chanzo cha nishati ila iwapo mtu atakula kiwango kikubwa hubadilishwa na kuwa mafuta.

“Pia, tuepuka kula nyama nyekundu kwa wingi. Nyama pendekezwa kwa umri wetu ni samaki na kuku. Nyama nyekundu ina mafuta ya lehemu nyingi huharibu mishipa ya damu na ikiliwa kwa wingi huweza kupelekea kupata saratani hususan ya utumbo mpana,” amesema Dk Lugina na kuongeza:

“Kwa umri wetu tunashauriwa pia kula vyakula vya mbogamboga na matunda kwa wingi na chumvi kidogo sana.

 

“Pia, tunywe pombe kwa kiasi; tuepuka unene ulipindukia.Unene ni chanzo kikubwa cha shinikizo la juu la damu na saratani.

“Umuhimu wa kufanya mazoezi; mazoezi ni muhimu sana katika umri wetu ili kutukinga na maradhi. Inapendekezwa mazoezi yafanyike walau dakika 20 kila siku. Mazoezi pendekezwa ni mazoezi ya kujenga pumzi kama kukimbia na kwa kiasi kidogo ni mazoezi ya kujenga misuli.

“Kuepuka sigara; sigara ni sumu. Ni chanzo kikubwa cha matatizo ya moyo na saratani.

“Kujijengea tabia ya kupima afya; katika umri wetu tunanyemelewa na saratani na magonjwa ya moyo kama shinikizo la juu la damu.

“Tujenge utaratibu wa kupima shinikizo la damu na tukifika miaka 50 tutaanza kupima saratani ya tezi dume walau moja kwa mwaka.

“Pia tuwahimize wake zetu wakapime saratani ya matiti na shingo ya uzazi. Huduma hizi ni bure kabisa Hopsitali ya Ocean Road.”

Baada ya kutupitisha katiba na kanuni zake ya Tambaza Alumni93, ilifuata kazi ya kutunuku baadhi ya watu waliofanikiwa.

Tuzo ya ubunifu alipewa Godfrey Woisso, Dk Hussein Kitta (Heshima), Mapinduzi Mwankemwa (Uchambuzi), Dk Clement Mugisha (Mafanikio) ambaye ni daktari bingwa wa upasuaji Neuro Surgeon Specialist Hospitali ya Taifa Muhimbili kitengo cha Mifupa (Moi) na Zaki Muhidin (Kujitolea).

 

Chanzo: mwananchi.co.tz