Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wahitimu darasa la saba wapewa neno

Darasa La Saba.jpeg Wanafunzi wakiwa kwenye mahafali

Sat, 24 Sep 2022 Chanzo: Mwananchi

Wanafunzi wa darasa la saba, wametakiwa kujitahidi katika mitihani yao ya mwisho ya kuhitimu elimu ya msimngi ili kuwawezesha kuendelea na masomo ya sekondari.

Wito huo umetolewa leo Jumamosi, Septemba 24, 2022 na afisa elimu vifaa na takwimu wa Wilaya ya Ubungo, jijini Dar es Salaam, Bundala Malando katika mahafali ya nne shule ya awali na msingi ya Taasisi ya Elimu Ebonite.

Malando amewaasa wahitimu hao 22 ambao watafanya mitihani yao ya taifa, Oktoba 5 na 6, 2022 kujichunga na kujiepusha na tabia hatarishi ambazo zitafanya wakatishe ndoto zao.

"Wanafunzi muongeze bidii katika masomo, hapa mjini yapo mambo mengi na muombe Mungu awajalie afya ya mwili pamoja na akili," amesema Malando

Amesema katika kipindi hiki, wanafunzi wafanye mapitio yayale waliyojifunza kwa kushirikiana na walimu.

"Muda mwingi watoto wamekuwa shule, sasa wanarudi nyumbani wazazi tuwe makini, kusimama imara kusudi watoto wetu waweze kufikia malengo yao,” amesema

Katika mahafali hayo kulikuwa na maonyesho mbalimbali ikiwa ni pamoja na ngoma za makabila mbalimbali, lugha ya alama, maonyesho katika somo la sayansi na hisabati.

Pia katika taasisi ya Elimu ya Ebonite hutolewa mafunzo ya lugha mbalimbali za kigeni ikiwa ni pamoja na Kichina, Kifaransa na mafunzo ya ukalimani.

Katika mahafali hayo wanafunzi walionyesha vipaji vingi ikiwa ni pamoja na kuimba, kucheza muziki, pamoja na maonyesho ya mavazi kama tamaduni za wa Afrika.

Awali, mwalimu mkuu wa shule ya awali na msingi ya Ebonite, Bahati Nickson amesema mafanikio waliyoyapata tangu kuanzishwa kwa shule hiyo yenye wanafunzi 250 ni kuongeza kwa wanafunzi kila mwaka.

"Shule ilianza na watoto 13 hadi sasa tunao watoto 250 na wahitimu 22 kwani wameandaliwa kitaaluma na kimaadili," amesema Nickson.

Alisema wanafunzi wamefaulu vizuri mitihani yao ya kujipima na kuwa na matokea mazuri ambayo wanafunzi 20 walipata daraja A na wawili walipata B matokea haya yametokana na kazi nzuri kutoka kwa walimu na walezi wa watoto wetu.

Naye Prince Godfrey, mhitimu wa darasa la saba akizungumza kwa niaba ya wenzake amesema, wanaushukuru uongozi wa shule kwani wanamaliza elimu ya msingi na kuendelea na elimu ya sekondari kadri Mungu atakavyowajalia.

"Haikuwa rahisi kwani bila msaada wa walimu wetu na Mungu hivyo nidhamu, kumcha Mungu na kujituma ndio msingi hadi sasa nina karibia kumaliza hatua hii ya kwanza," amesema Godfrey.

Chanzo: Mwananchi