Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wahamiaji haramu 21 wadakwa

Fri, 24 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Morogoro. Wahamiaji haramu 21 wanashikiliwa na polisi mkoani Morogoro baada ya kukamatwa maeneo mbalimbali mkoani humo.

Baadhi baadhi yao walikutwa katika mabasi ya abiria wakiwa wamevaa sare za vyama vya siasa na kujifunika mashuka ya kimasai. Uvaaji wa mavazi hayo ni ili wasitambulike kirahisi wakati wakiingia nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Agosti 24, 2018 naibu kamishna wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Morogoro, Safina Muhindi amesema walibaini mbinu hiyo na kuweka mtego wa kuwakamata.

Amewataka wananchi kuwafichua watu wanaowatilia mashaka kwa maelezo kuwa wamekuwa wakiliingiza Taifa hasara, ikiwa ni pamoja na kujihusisha na matukio yanayohatarisha usalama na amani.

Pia, aliwaonya wenye mabasi kuwa makini akiwataka kujiridhisha kila abiria wanaowapakia katika mabasi yao na kusisitiza kuwa sheria haitamuacha mtu salama.

Chanzo: mwananchi.co.tz