Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wahamaiaji haramu 1,152 wakamatwa Kagera

FUSSY Wahamaiaji haramu 1,152 wakamatwa Kagera

Wed, 3 Nov 2021 Chanzo: eatv.tv

Jumla ya wahamiaji haramu 1,152 wamekamatwa na Idara ya Uhamiaji mkoani Kagera, katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia Agosti hadi Oktoba mwaka huu, baada ya kubainika kuingia kinyemela katika maeneo mbalimbali mkoani Kagera.

Akizungumza na waandishi wa habari juu ya namna gani idara hiyo inakabiliana na tatizo la watu wasio raia kuingia hapa nchini bila kufuata utaratibu, Mkuu wa Uhamiaji mkoa wa Kagera Thomas Fussy, amesema kuwa wahamiaji 1,133 wamerejeshwa nchini mwao na wengine tisa wamefikishwa mahakamani.

Fussy amesema kuwa wamefikia uamuzi wa kurejesha idadi kubwa ya wahamaji hao nchini mwao ili kuepusha kuongeza msongamano katika magereza, kutokana na uwepo wa ugonjwa wa COVID-19.  

Chanzo: eatv.tv