Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wagonjwa wafulishwa mashuka ya hospitali Mtwara

B138FDBB 612E 4617 8B88 943A591F35C6.jpeg Wagonjwa wafulishwa mashuka ya hospitali Mtwara

Sat, 26 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ukosefu wa maji katika Kijiji cha Chihangu kilichopo Wilaya ya Newala, Mkoa wa Mtwara umesababisha wagonjwa wanaotibiwa katika Kituo cha Afya Chihangu kutakiwa kufua nguo za hospitali kabla ya kuruhusiwa.

Mkazi wa Kijiji cha Kihangu B, Musa Kajana amesema wagonjwa wanapomaliza kupata matibabu wamekuwa wakitakiwa na kituo hicho cha afya kufua shuka wanazozitumia ili waziache zikiwa safi.

“Huwezi kuruhusiwa hapa mpaka ufue shuka kwa kutumia maji yako ndio uyarudishe, shuka zinakuwa hazina madhari nzuri sababu ya uchafu, ndio maana wagonjwa wanakataa kutumia shuka za hapa,” amesema Kajana.

Wananchi hao wameeleza kero wakati wakipokea msaada wa mashuka 100 na vitanda kumi na magorodo kumi vyenye thamani ya Sh7 milioni vilivyotolewa na Benki ya NMB wilayani Newala.

Mkuu wa kituo hicho, Dkt Anthony Rioba amesema wakati wa changamoto ya maji waliwaomba wagonjwa hususan wale wa upasuaji kusuuza nguo za hospitali ambazo zinakuwa zimechafuka damu na uchafu mwingine kisha wao hospitali huzifua kwenye mashine na dawa.

Waziri wa nchi, ofisi ya Rais, (kazi maaluum), George Mkuchika ambaye amepokea msaada huo kutoka NMB amesema Serikali imetoa kiasi cha Sh84 bilioni kwa ajili ya kukarabati mradi wa makonde na tayari wakandarasi wapo kazini wilayani Newala.

“Kwa hiyo ndugu zanguni kwa shida ya maji ilivyotusumbua sasa neema inakuja, mradi wa Makonde ni wa muda mrefu toka mwaka 1953 mitambo imechoka, mabomba yameoza na uzalishaji umekuwa mdogo sana”.

Mkazi wa Chihangu, Celestine Nandonde, ameiomba Serikali kuharakisha mradi huo ili msaada wa mashuka uliotolewa na NMB uwe na manufaa na yaweze kuwa katika hali nzuri.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live