Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafugaji waomba msaada wa Magufuli nyumba 34 zikichomwa moto

Tue, 27 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Wakazi wa kijiji cha Vilima Vitatu kata ya Nkaiti Wilaya ya Babati wamemwomba Rais wa Tanzania, John Magufuli kuingilia kati sakata la nyumba zao 34 kuchomwa moto.

Akizungumza leo Jumanne Agosti 27, 2019, Juma Kwanjay amesema licha ya agizo la Rais Magufuli la kupiga marufuku wafugaji kunyanyaswa kwenye maeneo yao, bado wanakumbana na wakati mgumu.

Amesema kumekuwa na matukio ya mara kwa mara ya wafugaji kuondolewa kwa nguvu kwenye maeneo yao na kwamba nyumba hizo walikuwa wakiishi watu 150.

“Waziri wa Mifugo na Uvuvi (Luhaga Mpina) Julai 29, 2019 alifika katika kijiji cha Vilima Vitatu na kuagiza katika mkutano wa hadhara kuwa wafugaji na wavuvi wasiondolewe kama Rais Magufuli alivyoagiza,” amesema Kwanjay

Mkazi wa kijiji hicho, Dorcas Bayay amesema, “Hatulali mchana na usiku, watoto wanaugua kutokana na baridi na wanalala chini, kwa nini tunakuwa kama wakimbizi katika nchi yetu wakati wapo viongozi walioteuliwa  kulinda watu na mali zao.”

Kauli hiyo iliungwa mkono na mkazi mwingine wa kijiji hicho, Gidajur Gwaidanyi aliyebainisha kuwa kuondolewa katika yao kumesababisha mifugo yao kupotea.

Pia Soma

 

Chanzo: mwananchi.co.tz