Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyakazi wanne Green Miles wakamatwa na polisi

92647 Pic+green Wafanyakazi wanne Green Miles wakamatwa na polisi

Wed, 22 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Longido. Wafanyakazi wanne wa kampuni ya uwindaji ya Green Miles iliyoondolewa katika kitalu cha Lake Natron(east) wilayani Longido wanashikiliwa na polisi kwa madai ya kukaidi agizo la Serikali ya Tanzania kuwaondoka wa hiari katika kitalu hicho.

Wafanyakazi hao wamekamatwa na polisi leo Jumatano Januari 22, 2020 waliokuwa wameongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Longodo mkoani Arusha.

Wanatuhumiwa kuendelea na kazi katika kitalu hicho licha ya kutakiwa kuondoka Januari 20, 2020.

Katibu tawala Wilaya ya Longido, Toba Nguvila amesema baada ya wafanyakazi hao kukamatwa, eneo hilo litakuwa chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (Tawa) kwa kushirikiana na polisi.

“Tumetekeleza maagizo ya Serikali kuiondoa kambini kampuni hii kutokana na migogoro iliukuwepo,” amesema.

Ofisa wanyamapori wa kikosi cha kuzuia ujangili Mkoa wa Arusha, Emmanuel Pius amewataja wanaoshikiliwa kuwa ni kaimu meneja wa kambi ya Tandala, Lazaro Lembrise, Moses Sikange, Mohamed Bembe na  Hassan Mahonza.

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement
"Wanashikiliwa kwa tuhuma za kukaidi amri halali ya Serikali,  na polisi ndio wanafanya uchunguzi wa tukio hili na wakikamilisha watafikishwa mahakamani,” amesema.

Agosti 7, 2019 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla alitangaza uamuzi wa Serikali kuiondoa kampuni hiyo kutokana na kukiuka taratibu za uwindaji.

Hata hivyo, kampuni hiyo iliomba kuongeza muda hadi Desemba 16, 2019 ili kukabidhi kitalu hicho kwa madai wakati uamuzi unatangazwa walikuwa na watalii wakiwinda.

Jana Lembrice alilieleza Mwananchi kuwa hawana taarifa kutoka kwa mkurugenzi wao, Awadhi Abdalah aliyopo nje ya nchi kuwa wanatakiwa kuondoka katika kitalu hicho.

“Tulipata taarifa kupitia vyombo vya habari na katika ofisi ya Dar es Salaam kwamba kuna matangazo kutakiwa kuondoka lakini hatukupewa maelekezo na uongozi,” amesema Awadh.

Chanzo: mwananchi.co.tz