Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyakazi waandamana wakidai mishahara

10099 Kuandmaan+pic TZW

Wed, 27 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Waliokuwa wafanyakazi wa Sahara Media, leo Juni 26 wameandamana kwenda makao makuu ya ofisi hizo jijini Mwanza wakishinikiza uongozi kuwalipa fedha zao za mishahara baada ya kuachishwa kazi bila malipo kwa kipindi kirefu.

Wakizungumza nje ya ofisi hizo zilizopo Ilemela jijini hapa, baadhi ya wafanyakazi hao, Simba Julius Bukombe amesema wapo zaidi ya wafanyakzi 90 waliositishiwa mikataba ya kazi tangu Machi mwaka huu wakidai zaidi ya Sh700 milioni lakini kila wanapodai fedha zao imekuwa ni kupigwa chenga na mwajiri.

“Tunaonekana kama hatufahi, baada ya kuachishwa kazi tuliambiwa tutapewa fedha zetu lakini kila wakati tunapodai imekuwa ni mizunguko kejeli na dharau, sasa tumechoka tunachotaka ni haki yetu,” amesema Julius.

Aliyekuwa mfanyakazi mwingine Loyce Lubango amesema: “Sisi pia tuna familia zinazotutegema sasa ni zaidi ya miezi minne hamjui tunaishije, tunakula nini na familia inakula wapi, kwakweli hili ni jambo la udhalilishaji.”

Kwa upande wake, Meneja wa Utawala wa Sahara, Raphael Shiratu amesema jambo hilo linashughlikiwa.

Chanzo: mwananchi.co.tz