Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyakazi wa SGR, askari JWTZ wafariki ajalini

65720 Pic+sgr

Sat, 6 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Morogoro. Wafanyakazi wanne wakiwamo wafanyakazi wa kampuni ya Yapi Markezi inayojenga reli ya kisasa “SGR’ na askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wamefariki dunia papo hapo baada ya magari mawili waliyokuwa wakisafiria kugongana eneo la Ubena Zomozi barabara ya Morogoro- Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Julai 5, 2019, kaimu mganga mkuu wa hospitali ya furaa mkoa wa Morogoro, Dk Fransis Semwene amewataja waliofariki ni Modriki Mwaisyupa (41), Inocent Maiko (37) ambao ni wafanyakazi wa kampuni ya Yapi Markezi.

Dk Semwene amewataja wengine ni sema Zainabu Shija (32) aliyepewa lifti pamoja na Askari wa JWTZ kikosi cha Ngerengere aliyefariki jina lake halikuweza kufahamika

Amesema miili mitatu ilipokelewa katika hospitali hiyo na kuhifadhiwa huku mwili wa askari wa JWTZ ulipelekwa hospitali ya Jeshi Ngerengere kwa ajili ya taratibu za kijeshi.

Amesema baada ya miili hiyo kupokelewa hospitalini hapo taratibu za kuifanyia, uchunguzi wa kidaktari zinafanywa na baadaye ndugu watakabidhiwa kwa ajili ya mazishi.

Mwananchi limemtafuta Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, Wilbrod Mutafungwa kupata undani wa mazingira ya ajali ilivyokuwa ambapo alisema ajali hiyo ilitokea eneo la mkoa wa Pwani hivyo hawezi kuwa na taarifa hizo.

Pia Soma

Naye kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa alipoulizwa kuhusu ajali hiyo amesema yeye binafsi hana taarifa zozote na kwamba askari wake wamefuatilia lakini hawajapata taarifa za ajali hiyo.

Chanzo: mwananchi.co.tz