Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyakazi mradi wa SGR wagoma, siku nne hakuna kazi

SGR 1 Wafanyakazi mradi wa SGR wagoma, siku nne hakuna kazi

Mon, 10 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Sisi Wafanyakazi tunaofanya kazi katika Mradi wa SGR Kituo cha Itigi Rot 2 Camp, Kampuni ya Yap Merkez ambao tunatengeneza Kilometa 150 tumeamua kuingia katika mgomo huo kutokana na maslahi duni hasa kwa wazawa.

Mgomo huo ulianza kwa walioingia usiku wa jana tarehe 6 mwezi wanne 2023 na sisi ambao tumeingia asubuhi tunaendelea kwa kuwa tunataka haki itendeke.

Huku kinachoendelea baadhi ya viongozi wa SGR wamekusanyika hapa kuzungumza na wawakilishi wetu ambao ni wafanyakazi lakini bado muafaka haujafikiwa.

Hali halisi ipo hivi sisi vibarua wa chini mbali na kuwa hatuliwpi kwa wakati na tunapolikwa hakuna usawa, pia hatupati chakula wala maji tofauti na wageni ambao wao wanapata stahiki zote na malipo yao ni makubwa.

Tumeshalalamika sana kuhusu suala hili, tunafanyakazi muda mwingi zaidi ya wageni lakini bado wanatulipa kidogo na hakuna malipo ya overtime.

Kwa jumla sijui hesabu kamili ya vibarua tulioko japa lakini ni zaidi ya 200 au 300, tunaiomba Serikali kuwa tunajua ina nia nzuri lakini kuna watu wachache wanataka kutumia nafasi hiyo kuharibu mambo na kutukandamiza sisi watu wahali ya chini ambao ndio tunaofanya sana kazi.

Kwa kuwa tunawasiliana na wenzetu wa vituo mbalimbali, tumeambiwa Tabora napo mambo si mambo, nasikia nao wamegoma kutokana na sababu kama hizi.

Unajua wao wanafikiri vibarua wote hatujasoma au elimu yetu ni ya chini, wengine tumekuja huku kwa kuwa tu maisha ni magumu mtaani ndio maana tumeona badala ya kuingia mtaani na kufanya mambo ya ajabu, tuje kufanya kazi za halali kwa faida ya nchi.

Mgomo wetu hauna maana ya kutaka kuharibu mradi lakini lengo ni kuwa tuwe wazalendo lakini tutendewe haki.

===========

Inadaiwa baada ya mgomo huo kuanza tangu Aprili 6, 2023, viongozi wa Yap Merkez wakazungumza na wafanyakazi hao kwa ajili ya kupata utatuzi wa changamoto husika.

Lakini hadi kufikia Jumamosi Aprili 8, 2023 hakukuwa na muafaka baina ya pande mbili, ndipo jana Aprili 9, 2023 kikao kingine kikafanyika na uongozi wa Yap Merkez ukatoa ahadi kadhaa kuwa kufikia Aprili 20, 2023 kuna malipo yataanza kutolewa kama mahitaji ya waliogoma yanavyotaka.

Inaelezwa kuwa hali hiyo angalau ikatuliza hasira za waliogoma, makubaliano yaliyofikiwa ni kuwa leo Aprili 10, 2023 warejee kazini wakati huo walichokubaliana kinafanyiwa kazi.

============

Mkurugenzi wa Kitengo cha Uhusiano wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Jamila Mbarouk alipoulizwa juu ya suala hilo la mgomo amesema "Hii inanilimit kuielezea kwa kuwa wahusika ni mkandarasi Yapi Merkez."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live