Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyakazi Kigamboni kuhamia nyumba mpya

7cfafc1518de64f1b669285cbdf70194 Wafanyakazi Kigamboni kuhamia nyumba mpya

Wed, 20 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

UJENZI wa nyumba za wafanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigamboni umekamilika kwa asilimia 90 na kuna uwezekano wa kuanza kutumika mwezi ujao.

Ujenzi wa nyumba hizo umetokana na agizo la Rais John Magufuli alilolitoa wakati alipozindua wilaya hiyo mpya Februari 11, mwaka jana.

Akizungumza na HabariLEO jana, Mkuu wa wilaya hiyo, Sara Msafiri alisema ujenzi wa nyumba zote 24 umeshakamilika na kuwekewa huduma zote muhimu zinazotakiwa.

“Kwa sasa kinachongojewa ni kuvutwa kwa maji kuelekea kwenye eneo hilo, ambapo kwa sasa mchakato wake umeshaanza kushughulikiwa.”

“Kwa sasa barabara kuelekea kwenye eneo hilo pamoja na zile zilizopo ndani ya eneo zinaendelea kuchongwa ili kuwawezesha wafanyakazi kuingia na kutoka kirahisi katika makazi yao hayo.”

“Ninachojivunia kwa sasa ni kuwa kazi nzuri inaendelea kufanywa na wajenzi ambao ni Jeshi la Polisi na kwa sasa wanakaribia kumaliza, hata tukihamia leo tunaweza kuendela kuishi tu ila kwa sasa wacha wakamilishie suala la maji,” alisema Msafiri.

Alisema makazi hayo yapo karibu na ofisi za halmashauri hiyo hivyo itakuwa rahisi kwa wafanyakazi kuwahi kazini na kufanya kazi kwa amani kutokana na kutokuwa na hofu ya mahala pa kuishi.

Chanzo: habarileo.co.tz