Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyakazi East Coast Oils wagoma, wadai kulipwa fedha kiduchu

Tue, 12 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wafanyakazi zaidi ya 100 wa Kampuni ya East Coast Oils and Fats Limited iliyopo Shimo la Udongo jijini Dar es Salaam, wamegoma kufanya wakidai kunyanyaswa na uongozi sambamba na kulipwa fedha kidogo isiyoendana na majukumu yao ya kazi.

Wafanyakazi hao wamegoma leo Jumatatu Februari 11, 2019 wakitaka msimamizi wao, Herry Simila kuondolewa kwa maelezo kuwa anawatolewa maneno ya kashfa pale wanapompelekea matatizo yao.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Ashura Mussa amesema wamekuwa wakifanya kazi katika mazingira magumu lakini wanalipwa fedha kidogo ambayo haiendani na kazi wanazozifanya.

Wamesema kutokana na kulipwa fedha kupitia benki makato yamekuwa makubwa, “hatutaki kulipwa fedha hizo kupitia benki kwa sababu fedha yenyewe tunayolipwa ni kidogo haiwezi hata kukidhi mahitaji yetu. Hivyo tunataka fedha zetu hizo zilizopotea turejeshewe.

John Lucas amesema Simila anapaswa kuondolewa kwa maelezo kuwa mfanyakazi akiwa na tatizo hamsaidii.

Issa Lupangile, mkurugenzi wa operesheni wa kampuni  ya Upami Group Limited inayowasimamia wafanyakazi hao wanaolipwa ujira wa Sh7,500 kwa siku amewaahidi  ifikapo Februari 28, 2019 watatatuliwa matatizo yao.

Lupangule aliwataka wafanyakazi hao kuacha mgomo na kuendelea na kazi, baadhi walikubali na kuendelea na kazi na wengine waligoma na kutawanywa na polisi waliokuwepo eneo hilo.

Kwa upande wake Simila amesema madai ya wafanyakazi hao si ya kweli, akibainisha jinsi anavyokuwa nao bega kwa bega ikiwa ni pamoja na kuwasaidia wanapopata matatizo.



Chanzo: mwananchi.co.tz