Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyakazi ATCL wafanya matembezi kuimarisha afya

Mon, 15 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wafanyakazi wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) wamefanya matembezi ya afya kutoka zilizopo ofisi zao Posta jijini Dar es Salaam hadi viwanja vya Shule ya Seminari ya Al Muntazir ambapo walicheza mchezo wa kirafiki wa mpira wa miguu dhidi ya Benki ya Uwekezaji Tanzania (TIB).

Matembezi hayo yamefanyika leo Jumamosi Aprili Mosi, 2019 na Mkurugenzi wa ATCL Ladislaus Matindi amesema ni utaratibu wa kawaida wa shirika hilo kufanya mazoezi kila mwisho wa juma moja kwa mwezi.

"Tunafanya mazoezi kama haya kulinda afya zetu, na kuimarisha mshikamano, viongozi katika shirika wanapata nafasi ya kubadilishana mawazo na wanaowaongoza si mambo ya kiofisi tu bali hata maisha binafsi," amesema Matindi.

Ameongeza mazoezi ni muhimu katika maisha ya binadamu na Watanzania wakiwa na utamaduni wa aina hii watapata fursa nzuri ya kujenga taifa lao.

Mchezaji nguli wa soka wa zamani, Mohammed Hussein ambaye alijiunga na matembezi hayo amesema kinachofanywa na shirika hilo kinapaswa kuigwa na mashirika mengine na taasisi za hapa nchini.

"Mazoezi ni kinga ya maradhi nyemelezi, ni muhimu baada ya kazi za kukaa ofisini muda mrefu watu wakapata nafasi ya kufanya mazoezi, si lazima yawe makubwa sana lakini walau kutembea Kilometa mbili kwa siku," amesema mchezaji huyo wa zamani wa klabu ya Yanga, Simba na Taifa Stars.



Chanzo: mwananchi.co.tz