Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyakazi 11 NMB wazama baharini, mmoja afariki dunia

71053 Pic+nmb

Wed, 14 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tanga. Wafanyakazi 10 wa Benki ya NMB tawi la Korogwe jijini Tanga nchini Tanzania wamenusurika kifo huku mmoja akifariki dunia baada ya boti ya Klabu ya Yatchi iliyopo Raskazone kuzama katika Bahari ya Hindi.

Ajali hiyo ilitokea jana Jumapili Agosti 11, 2019 wakati wafanyakazi hao wakienda Kisiwa cha Toteni kufanya utalii.

Meneja wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) mkoa wa Tanga, Christopher Mlelwa akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu Agosti 12,2019 amesema alifariki ni Patrick Kiungulia (53) ambaye alikuwa akitafutwa.

Amesema mfanyakazi huyo amepatikana kufuatia timu wa wazamiaji majini wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Jeshi la Polisi wakiongozwa na Kikosi cha Wanamaji wa Jeshi la Wananchi kuendesha shughuli ya uokozi kwa zaidi ya saa 16.

Mlelwa amesema ajali hiyo ilitokea jana Jumapili baada ya boti ya Klabu ya Yatchi iliyopo Raskazone iliyokuwa imewabeba wafanyakazi hao kupigwa na wimbi kisha kupinduka katika bahari ya Hindi.

"Hawa wafanyakazi walikuwa wakienda Kisiwa cha Toteni kufanya utalii ikiwa ni sehemu ya sherehe ya siku ya familia ya wana-NMB ndipo walipofika katikati boti ikapigwa na wimbi na kupinduka majini," amesema Mlelwa

Pia Soma

Naye Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Tanga, Edward Bukombe amesema boti hiyo ilikuwa na wafanyakazi wa NMB na familia zao 11 ambapo 10 kati yao waliweza kuokolewa kwa nyakati tofauti na kufikishwa hospitali ya mkoa wa Tanga ya Bombo kwa matibabu huku mmoja amepatika akiwa amefariki dunia.

Amewataka wanaotumia bahari ya Hindi kuwa makini katika kipindi hiki ambacho bahari imekuwa ikichafuka mara kwa mara ili kujiepusha na hatari za kupoteza maisha.

Chanzo: mwananchi.co.tz