Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyabiashara wanaopandisha bei vifaa vya ujenzi matatani

MJEMAA Wafanyabiashara wanaopandisha bei vifaa vya ujenzi matatani

Thu, 4 Nov 2021 Chanzo: ippmedia.com

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, amepiga marufuku wafanyabiashara mkoani humo, kupandisha bei holela ya vifaa vya ujenzi hasa katika kipindi cha ujenzi wa vyumba vya madarasa.

Amebainisha hayo leo wakati akipokea taarifa ya ujenzi wa mindombinu katika shule ya Sekondari Kishapu, ikiwamo ujenzi wa vyumba vya madarasa, kuwa changamoto kubwa ambayo ina wakabii ujenzi huo ni kupanda kwa bei ya vifaa vya ujenzi.

Amesema katika Mkoa wa Shinyanga, hataki kusikia mfanyabiashara yoyote kapandisha bei ya vifaa vya ujenzi ikiwamo Saruji, na kutaka wauze kwa bei ya kawaida, na wakiendelea kuuza bei juu watawashughulikia.

"Nakuagiza Kamanda wa Polisi Mkoa, Mfanyabiashara yoyote ambaye atabainika kupandisha bei ya vifaa vya ujenzi mchukulieni hatua, hatutaki mtu yoyote atukwamishe kwenye ujenzi huu wa vyumba vya madarasa," amesema Mjema.

"Sababu unapopandisha bei ya vifaa vya ujenzi, ina maana Mhe,Rais atuongezee tena fedha, hili sitakubaliana nalo, lazima bei iwe ya kawaida na siyo kutumia fursa kwenye ujenzi wa vyumba vya Madarasa," ameongeza.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya ujenzi wa miundombinu ya shule hiyo ya Sekondari Kishapu, Maburugi Samweli, akisoma Taarifa, alisema changamoto kubwa ambayo inawakabili kwa sasa katika ujenzi huo, ni upandaji wa bei ya vifaa vya ujenzi hasa Saruji na hivyo kufanya ujenzi kusuasua.

Aidha, amesema Saruji awali walikuwa wakinunua bei ya Sh. 19,500, lakini sasa wananunua Sh. 20,000 had 21,000,  Nondo za Milimita 12 walikuwa wakinunua Sh. 22,000,  na sasa wananunua Sh.27,000, kwa upande wa Mabati Geji 28 walikuwa wakinunua Sh.28,000, lakini kwa sasa wanauziwa Sh.35,000. 

Chanzo: ippmedia.com