Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyabiashara Kariakoo wawe watulivu

Moto Kariakooo.jpeg Wafanyabiashara Kariakoo wawe watulivu

Mon, 2 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa jumuiya ya Wafanyabiashara katika soko la Kariakoo Bw. Martin Mbwana ametoa wito kwa wafanyabiashara kuwa na utulivu wakati Serikali ikiendelea kutathmini hasara iliyopatikana na kuchunguza chanzo cha moto Kariakoo.

“Kikubwa ninacho omba ni utulivu Serikali ipo kama mlivyoona jana Mkuu wa Wilaya tulikuwa nae Mkuu wa Mkoa alikuja na viongozi wa mambo ya usalama wapo, tutulie tuangalie tathmini iliyoko hapa chanzo ni nini, cha moto huu na ili tulikomesha swala kama hili lisitoke tena eneo hili”

“Sasahivi kariakoo imeshakuwa kama ni fasheni flani ya moto kutoka kwenye eneo hili moto unatoka eneo lile, tukumbuke moto unavyotoka hivi inatupa hasara kubwa sana waliokuwa ndani ya soko na nje ya soko pia” amesema Bw. Mbwana.

Hata hivyo ajali za moto zikiendelea kujirudia maeneo ya masoko ikiwemo soko la Kariakoo husika, zitaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha moto huo ili kukomesha na kuzuia ajali kama hizo kutojirudia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live