Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyabiashara 3,000 wanahitaji vitambulisho Kigamboni

33816 Pic+kigamboni Tanzania Web Photo

Fri, 28 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam imesema inahitaji vitambulisho 3,000 zaidi kwa ajili ya kuwagawia wafanyabiashara wadogo kwa ajili ya kuwatambua.

Hayo yamesemwa leo Desemba 28, 2018 na mkuu wa wilaya hiyo, Sara Msafiri alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari na kuelezea mchakato wa ugawaji wa vitambulisho hivyo ulipofikia.

Sara amesema pamoja na kwamba hadi sasa wameshagawa asilimia 97 ya vitambulisho 5,000 walivyopatiwa kutoka kwa Rais John Magufuli, lakini wamegundua mahitaji yake ni makubwa.

"Huku Kigamboni tuna wafanyabiashara wa madafu ambapo asilimia kubwa yanayouzwa Dar es Salaam nzima yanatoka huko, tuna wafanyabiashara wa kokoto na wengine ambao wao hawazunguki bali wanakaa eneo moja.

"Hasa wote tunahitaji wawe na vitambulisho na kama tutapatiwa walau 3,000 kwa kuanzia tutashukuru," amesema Sara.

Kwa upande wake, Meneja wa Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Kodi Temeke, Gamaliel Mafie, amesema wamejipanga kutoka elimu kwa wafanyabiashara hao ili kuondokana na dhana ya kuwa vitambulisho hivyo vimelenga kuwakamua zaidi kwenye kutoa kodi.

Mafie amesema kuanzia Januari, 2019 wataanza msako wa kuwatambua watu ambao hawakuwa sahihi kuvipata vitambulisho hivyo na kuwarudisha katika kundi ambalo wanastahili.



Chanzo: mwananchi.co.tz