Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanya maombi kukemea Ebola

DININ Wafanya maombi kukemea Ebola

Mon, 7 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Viongozi wa dini mkoani Geita kwa kushirikiana na taasisi ya dini mbalimbali Tanzania interfaith partnership wamefanya mkutano wa maombi kwa ajili ya kukemea ugonjwa wa Ebola usiingie nchini.

Akiongea mara baada ya kumaliza maombi hayo mratibu wa TIP amesema wamefanya mkutano huo wa maombi ili kutoa elimu kwa kundi kubwa la watu ili wajikinge na ugonjwa wa Ebola.

"Tumeweka mkutano huu kwa ajili ya kutoa elimu kwa watu, tumetoa mafunzo kwa viongozi wa dini kama walivyosema, lakini tunatamani viongozi wa dini sasa wawafikishie watu ujumbe pamoja na kufanya maombi na viongozi wa dini mbalimbali katika mkoa wetu wa Geita basi wamekutanika mahali hapa kufanya maombi, tunafanya juhudi za kibinadamu lakini pia tunamuomba Mungu aweze kutuepusha na magonjwa haya hasa Ebola na Uviko19" amesema Azgard Stephen, Mratibu wa TIP  

Chanzo: www.tanzaniaweb.live