Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wadau wa pamba watoa maazimio 10

Sun, 22 Apr 2018 Chanzo: habarileo.co.tz

MKUTANO wa wadau na wawekezaji wa pamba, bidhaa za nguo na Mmavazi kutoka mikoa 17 inayozalisha zao hilo umeweka maazimio 10 ya kuboresha mnyororo wa zao hilo kuanzia kwa mkulima mzalishaji, mchakataji hadi mtengenezaji nguo nchini.

Akisoma maazimio hayo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Profesa Elisante ole Gabriel mjini Dodoma amesema, serikali ipo tayari kushirikiana na wadau hao kuhakikisha mnyororo huo tangu kuzalisha pamba hadi kutengeneza nguo unapata mafanikio makubwa.

Amesema wizara hiyo itaunda Kamati Maalumu itakayohusisha vijana wenye taaluma kutoka katika wizara hiyo ili kujifunza kutoka kwa wazee wazoefu waliopo katika sekta binafsi na hata kutembelea China kujifunza mifumo mbalimbali ukiwemo wa ulipaji kodi wa bidhaa zinazoingia nchini kutoka huko.

Profesa Ole Gabriel amesema katika suala la uingizaji bidhaa za nguo hafifu kutoka nchi mbalimbali hasa China, taasisi zinazohusika na udhibiti ikiwemo Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na nyingine zilizopo nchini zinatakiwa kusimamia na kuhakikisha kwamba bidhaa hafifu na zilizo chini ya kiwango haziingii katika soko la Tanzania.

Chanzo: habarileo.co.tz