Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wadaiwa kugeuza wanafunzi wapenzi

41847 Wamafinzi+pic Wadaiwa kugeuza wanafunzi wapenzi

Fri, 15 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Handeni. Baadhi ya walimu katika halmashauri ya mji wa Handeni mkoani Tanga wanatuhumiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanafunzi wao.

Wakichangia hoja ya masuala ya elimu kwenye kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya mji wa Handeni juzi, baadhi ya madiwani walisema wana taarifa kuwa kuna walimu wana uhusiano wa kimapenzi na wanafunzi na kutaka jambo hilo lichunguzwe na ushahidi ukipatikana wahusika wachukuliwe hatua kwani vitendo hivyo havikubaliki na ni kinyume cha sheria.

Diwani kata ya Chanika, Abdallah Chihumpu alisema wakati wao wakipambana kuongeza idadi ya wanafuzi na ufaulu, baadhi ya watu wanarudisha nyuma juhudi zao kwa vitendo kama hivyo.

“Wahusika wachukuliwe hatua haraka kwani kitendo hicho ni kinyume cha kanuni za kazi na wamekiuka maadidli kwani wao ni wazazi pia,” alisema.

Akichangia hoja hiyo, katibu tawala wilaya ya Handeni, Mwalimu Boniface Maiga alitoa onyo kwa mtumishi yeyote atakaebainika kujihusisha na kimapenzi na mwanafunzi atafukuzwa kazi na kuchukuliwa hatua za kisheria.

“Ni marufuku kisheria kwa mwalimu kuwa na uhusiano ya kimapenzi na mwanafunzi wa atakaebainika atapewa adhabu mbili kwa pamoja, kufukuzwa kazi na kufikishwa mahakamani,” alisema.

Alimpongeza mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Kenneth Haule kwa kuchukua hatua za awali baada ya kufahamishwa kuwa wapo walimu kwenye mji huo wanatabia hizo.

Kuhusu halmashauri kutofanya vizuri kwenye elimu, mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Twaha Mgaya alisema wameweka mikakati ya kufanya vizuri kwenye mihula ijayo, ikiwamo utoro kudhibitiwa na wazazi wasiowajibika kwa watoto wao kuchukuliwa hatua.



Chanzo: mwananchi.co.tz