Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wadaiwa kodi Mwanza kujieleza

5cba0666c730a9d1f0d0c8b4b1556edf Wadaiwa kodi Mwanza kujieleza

Tue, 18 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula amewataka wadaiwa wa kodi ya pango la ardhi katika jiji la Mwanza wandike barua kueleza lini watalipa fedha wanazodaiwa.

Jiji la Mwanza lina wadaiwa 123 wa kodi ya pango la ardhi wanaodaiwa takribani bilioni 2.2.

Dk Mabula amekutana na wanaodaiwa na wanaodaiwa kuanzia shilingi milioni 3 na kwa mujibu wa Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Mwanza Makwasa Biswalo jiji hilo linatakiwa kukusanya shilingi bilioni 6 ya kodi ya pango la ardhi .

Wadaiwa waliokutana na Dk Mabula waliahidi kulipa madeni na baadhi yao wameomba kulipa kwa awamu. Dk Mabula aliwataka wandike barua ikieleza azma hiyo na muda watakaokamilisha malipo.

"Kumiliki ardhi kumesisitizwa lakini pia kila mmiliki ajue wajibu wake wa kujua kulipa kodi na sisi tumeona badala ya kutumia sheria ya kuwafikisha mahakamani tuwaite tuwasikilize na kuwapa hamasa kulipa ili kumuwezesha Mheshimiwa Rais kufanya shughuli za kimaendeleo ikiwemo miradi mikubwa ya kimkakati" alisema Dk Mabula

Aliwataka wamiliki wanaodaiwa kodi ya pango la ardhi wasisubiri kushitakiwa katika mabaraza ya ardhi na nyumba ya wilaya na kubainisha kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha makusanyo yanapatikana ili kusaidia shughuli za kimaendeleo ikiwemo miradi ya kimkakati.

Alisema, baada ya kikao hicho watakaokaidi kulipa wataitwa kwenye mabaraza hayo na kwamba uamuzi wa huko ni aidha kulipa au mali za wadaiwa kunadiwa.

Wakati huohuo Dk Mabula amelitaka jiji la Mwanza na halmashauri nyingine nchini kuhakikisha zinatenga fedha kwa ajili ya kulipa fidia katika maeneo yaliyotwaliwa na Serikali kwa shughuli za umma.

Alisema, kuna baadhi ya maeneo ambayo halmashauri imeyachukua kwa ajili ya shughuli za umma lakini wamiliki wake hawajalipwa fidia na kusisitiza kuwa mamlaka hizo zitenge fedha katika bajeti zao kwa ajili ya kulipa fidia.

Pia Naibu Waziri wa Ardhi alizitaka halmashauri nchini zenye mipango kabambe kuacha kutoa vibali vya ujenzi kwenye maeneo bila kuzingatia mipango hiyo na kutolea mfano wa halmashauri ya jiji la Mwanza na Ilemela kuwa pamoja na kuwepo mpango unaoelekeza aina ipi ya ujenzi hufanyika bila kuzingatia na kusisitiza utoaji vibali vya ujenzi uzingatia mpango kabambe.

Chanzo: habarileo.co.tz