Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wachimbaji wa madini wafukiwa na kifusi Gairo

61854 Mgodi+pic

Mon, 10 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Morogoro. Wachimbaji wadogo ambao idadi yao bado haijafahamika wanahofiwa kufariki dunia baada ya kufukiwa na kifusi wilayani Gairo, mkoani Morogoro.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa wachimbaji hao wamefukiwa na kifusi cha mchanga wakati wakichimba madini aina ya dhahabu ambayo yameibuka siku za hivi karibuni katika Kijiji cha Iyogwe wilayani Gairo.

Akizungumza leo Jumapili Juni 9, 2019, Mwenyekiti wa chama cha wachimba madini Mkoa wa Morogoro, Dk Omary Mzeru amesema wamepata taarifa hizo na sasa wanafuatilia zaidi.

Mwananchi lilipomtafuta Mkuu wa mkoa  wa Morogoro, Dk Steven Kebwe amesema yeye na kamati yake ya ulinzi na usalama wanaelekea eneo la tukio.

Taarifa zaidi kuhusu tukio hili endelea kufuatilia Mitandao yote ya kijamii ya Mwananchi na MclDigital.

Chanzo: mwananchi.co.tz