Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wachimbaji madini wawili wafariki ndani ya shimo

49863 Pic+wachimbaji

Mon, 1 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tabora. Watu wawili wilayani Igunga mkoani Tabora wamekutwa wamefariki katika shimo walilokuwa wakichimba dhahabu.

Kamanda wa Polisi mkoa Tabora, Emmanuel Nley, akizungumza leo Jumatatu Aprili 1, 2019 amesema tukio hilo limetokea juzi saa nne usiku katika kijiji cha Matinje, kata ya Mwashiku, wilayani Igunga.

Kamanda Nley amesema wakazi hao, Jumanne Mayunga na mwenzake Benjamin Paul, waliingia katika shimo la mgodi wa dhahabu kwenye kijiji hicho na kuwasha moto kwa lengo la kupasua mawe wapate dhahabu.

Amebainisha kwamba wachimbaji hao wadogo walitumia mifuko ya nailoni ambayo ilisababisha kukosa hewa na kufariki dunia.

Kamanda huyo ameongeza kuwa miili ilichukuliwa na polisi kwa ajili ya uchunguzi na kisha kukabidhiwa ndugu zao.

Amewataka wachimbaji kuchukua tahadhari na kutumia utaalamu wanapochimba madini ili kuepuka madhara kama hayo ambayo yamesababisha vifo.



Chanzo: mwananchi.co.tz