Mirerani. Wamiliki na wachimbaji wa madini ya Tanzanite katika mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara wameiomba Serikali kuwapa mwaka mmoja ili waweze kuboresha miundombinu ya migodi yao ikiwemo kuweka uzio.
Wametoa tamko hilo baada ya baadhi ya migodi yao ambayo haina uzio iliyopo kitalu D na B (Opec) kuwekewa alama ya X ikitakiwa kuondolewa,, kuvunja au kufukiwa.
Wakizungumza katika kikao kilichofanyika leo Alhamisi Mei 23, 2019 wachimbaji na wamiliki hao wameomba muda huo ili kukamilisha kuweka sawa miundombinu.
Amos Makoy amesema wengi wao hawana fedha na kuomba muda huo ili kutekeleza agizo hilo.
"Wachimbaji wadogo wanahitaji kuwa wachimbaji wakubwa baada ya kupata madini hivyo tunaomba Serikali ituongezee muda wa mwaka mmoja ili tutekeleze hilo," amesema Makoy.
Mwenyekiti wa kamati ya Tanzanite, Money Yousuph amesema wachimbaji wamegawanyika kwenye matabaka tofauti kiuchumi hivyo wanaomba mwaka mmoja wa kutekeleza hilo.
Pia Soma
- VIDEO: Ndugai, mbunge Masele watuhumiana bungeni
- Mwanamke aua jambazi kwa kisu
- Zao la utomvu laiingizia Saohill Sh700 milioni
- VIDEO: Bunge la Tanzania lamsamehe Masele