Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wachimbaji 22 wafariki kwa kufukiwa na kifusi mgodinj

Mwe Shimoo49660 Picha mfano wa shimo mgodini

Sun, 14 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wachimbaji wadogo 22 wa madini ya dhahabu wamefariki dunia kufuatia ajali ya kufunikwa na ardhi katika Mgodi wa Ng'alita, Wilaya ya Bariadi, mkoani Simiyu.

Inaelezwa kuwa tukio hilo limetokea baada ya kudaiwa kuingia mgodini kwa kujipenyeza kinyume cha sheria kwani shughuli za uchimbaji zilikuwa zimesitishwa.

Kufuatia ajali hiyo iliyotokea saa 11 alfajiri Januari 13,2024 , Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kwa ndugu, jamaa na marafiki waliopoteza jamaa zao katika ajali hiyo na kwamba Vyombo vya ulinzi na usalama vikishirikiana na uongozi wa mkoa vinaendelea na juhudi za kutafuta miili mingine ambayo bado imekwama ndani ya kifusi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live