Baadhi ya wazazi wenye watoto wanaosoma Shule ya Msingi Matambarale wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi wamelalamika michango mingi shuleni hapo ikiwemo ya ujenzi wa vyoo bila kupewa risiti
Bakari Manzi mkazi wa Matambarale amesema kuwa kwenye Kijiji chao uongozi wa Kijiji umebuni njia ya kukusanya mapato ni kuchangisha wananchi michango ambayo haijadiliwi Wala kupitishwa na vikao halali, hivyo wanaiomba serikali kuingilia Kati Jambo hilo kwa ni limekuwa kero kwa wananchi.
"Tunaona serikali inatoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na vyoo na ilikataza michango ya ajabu lakini sisi kila kukicha michango na ukilipa upati hata risiti una andikwa kwenye daftari".amesema Manzi
"tumetangaziwa mchango wa shilingi elfu mbili Kila kaya kwa ajili ujenzi wa choo Cha shule, lakini mchango huyo hauna muda wa kukusanywa na kilichokusanywa wananchi hatupati taarifa ya mapato na matumizi wakati huo huo kamati inakusanya na kutumia"amesema Haji Mohamed
Haji Mohamedi Amesema kuwa michango hiyo imekuwa kero maana imekuwa mingi na inarudia rudia mara kwa mara.
Mwenyekiti wa kijiji Cha Matambarale kusini Mohamed Issa Ndogolo amesema utaratibu ulioko wa michango mara nyingi ni makubaliano na hupangwa na wananchi wenyewe, kwa niaba ya kamati ya shule.
Amesema ulifanyika mkutano wa Kijiji ambao ulipitisha azimio la Kila mwananchi kuchangia shilingi Elfu mbili kwa ajili ya ujenzi wa vyoo vya shule.
Amesema kwamba yeye binafsi amechangia lakini hajapata risiti kwa kuwa kamati haina kitabu Cha kukusanyia mchango wanatumia daftari la kawaida.
Kwa upande Mkurungezi Mtendaji wa Halmshauri hiyo Frank Chonya amesema kuwa hana taarifa kwamba Kuna wazazi wanachangishwa michango kwa ajili ya ujenzi wa vyoo; kwamba atafutilia kujua juu ya hilo.
"Tuna fedha za ujenzi wa madarasa na vyoo nashangaa kusikia kuna wananchi wanachangishwa michango nitafuatilia kujua hilo"amesema Chonya.