Dodoma. Makamu wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan Oktoba 27, 2019 atafungua semina ya wajumbe wa chama cha wabunge wanawake wa mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika itakayofanyika jijini Arusha.
Akizungumza leo Jumatano Oktoba 23, 2019 Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema semina hiyo itawakutanisha washiriki 50 kutoka nchi 18 za Jumuiya ya Madola.
Nchi hizo ni Afrika Kusini, Botswana, Cameroon, Eswatini, Ghana, Kenya, Lesotho, Malawi, Mauritius, Msumbiji, Nigeria, Namibia, Rwanda, Sierra Leone, Seychelles, Tanzania, Uganda na Zambia.
“Kauli mbiu katika semina hiyo ni kuboresha ushiriki wa wanawake katika michakato ya uchaguzi,” amesema.
Amesema miongoni mwa malengo ya semina hiyo ni kuboresha ushiriki wa wanawake katika mchakato ya uchaguzi ili kuongeza idadi ya wanawake katika vyombo vya maamuzi.
“Zipo changamoto nyingi zinazowakwamisha wanawake kushiriki mchakato ya uchaguzi kama wapiga kura na wagombea. Changamoto hizo zote pamoja na namna ya kuzitatua zitajadiliwa katika semina hiyo,” amesema.
Pia Soma
- Baba aeleza mauaji ya mwanaye yalivyokatisha ndoto kuwa muuguzi
- KAKAKUONA: Tunasubiri Rais afoke ndiyo mambo yaende?
- MAKALA YA MALOTO: Kuhamia Dodoma kumbukumbu halisi kumuenzi Mwalimu Nyerere
- Maendeleo na uwajibikaji, ushirikishaji na uwezeshaji
Amesema uwakilishi wanawake katika baraza la madiwani nchini ni asilimia 30, wabunge (36.6), mawaziri 11 kati ya 45 na majaji ni 19 kati ya 88.