Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wabunge wa Ilala, Segerea wajadili ilani ya CCM , Changamoto lukuki zatajwa

Sun, 26 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wabunge wawili wa Majimbo ya Ilala na Segerea leo Mei 25, 2019 wamewasilisha taarifa za utekelezaji wa Ilani ya CCM 2015/20 huku changamoto kadhaa zikiwekwa wazi.

Mkutano huo umehudhuriwa na Mwenyekiti wa CCM, Mkoa, wabunge, viongozi wa CCM Mkoa, wajumbe wa mkutano Mkuu wa Kata, wajumbe wa halmashauri kuu ya Chama hicho na wenyeviti wa Mitaa.

Katika taarifa ya Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu amesema Jimbo hilo lina wakazi 200,000 tu ila wafanyabiashara ni milioni 2.6 ,hatua inayoathiri upatikanaji wa huduma ya Afya kwa idadi hiyo.

"Wote wanahitaji huduma za Ilala, kwa utaratibu dawa zinaletwa Kwa idadi ya wakazi hao laki mbili, tuna hospitali kubwa ya Mnazi mmoja, tunalishughulikia ,tutawafukuza wagonjwa," amesema Zungu.

Zungu amesema changamoto ya gharama za kutoa maiti imekuwa kero kwa wananchi wasiokuwa na uwezo, akidai kulishughulikia.

Kuhusu Elimu, Zungu amesema hakuna shule isiyokuwa na huduma za maji licha ya changamoto ya uchakavu wa majengo ya shule na nyumba za walimu, pamoja na uhaba. 

Pia Soma

Kuhusu barabara, Zungu amesema bado kuna changamoto kubwa inayowaliza madiwani katika vikao.

Amesema kwa sasa wanapambana na utekelezaji wa miradi ya barabara angalau 15 zitakazosaidia kupunguza asilimia 60 ya foleni zinazopatikana katika mipaka ya Jimbo hilo.

Ametaja maeneo yenye changamoto hiyo ni pamoja na Kisutu, mchikichini na Kata ya Ilala.

Akiwasilisha taarifa yake ya Jimbo la Segerea, Mbunge Bonnah Kamoli amesema Kata zote 13 zimeunganishwa huduma ya maji isipokuwa baadhi ya Mitaa, hadi kufikia 2020 itakuwa yote tayari au kufikia asilimia 90.

Jimbo hilo lenye mitaa 60, lina shule 34 za msingi na idadi ya Wanafunzi inaongezeka kila mwaka.

Anasema kuhusu miundombinu, maeneo mengi yako vizuri lakini ujenzi wa barabara ya Kimanga unasuasua huku wakazi wa Kiwalani na Minazi marefu wakiishi kama wapo kisiwani.

Kuhusu Afya, Bona amesema ongezeko la wakazi wanaofikia 1,010, 000 imekuwa changamoto ya msongamano wa watu katika hospitali ya rufaa ya Amana.

"Kwa sasa tunajenga kituo kikubwa cha Plan International katika Kata ya Mnyamani na pia tunapanua huduma katika baadhi ya vituo," amesema.

Chanzo: mwananchi.co.tz