Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waathirika wa tope la Mgodi wa Almasi wadai fidia

Tope La Mgodi Wa Almasi Waathirika wa tope la Mgodi wa Almasi wadai fidia

Sat, 3 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakazi wa Kata ya Mwaduilohumbo Mkoani Shinyanga ambao Nyumba na Mashamba yao yalifunikwa na tope la Bwawa Mgodi wa Williamson Diamond kupasuka, wameiomba Serikali kuharakisha tathmini ya uharibifu ili walipwe fidia.

Bwawa la Maji machafu la Mgodi wa Williamson Diamond lilipasuka Novemba 7, 2022 na tope kusambaa kwenye Makazi ya watu ambapo Kaya zaidi ya 30 zenye Wakazi 145 ziliathiriwa.

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Joseph Mkude, amewataka Wananchi hao kuwa wavumilivu wakati zoezi la tathmini likiendelea huku akiwataka kutoa taarifa sahihi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live