Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waandishi wa Habari wafariki kwa ajali Pwani

Asdwd Waandishi wa Habari wafariki kwa ajali Pwani

Tue, 26 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waandishi wa habari wawili wa mkoa wa Lindi wamefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokeajana usiku wa kuamkia leo Machi 26, 2024 katika eneo la Nyamwage mkoani pwani

Wanahabari hao walikuwa wanatokea jijini Dar es Saalam kuelekea mkoani Lindi ambapo walipata ajali saa saba usiku leo hilo.

Akizungumza kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa kipolisi Rufiji, SACP Protas Mutayoba amesema chanzo cha ajali hiyo ni gari walilokuwa wakisafiria kugongana na lori eneo la Nyamwage.

"Waliofariki ni mwandishi wa habari wa kampuni ya Sahara Media group, Josephine Kibiriti na Abdalah Nanda wa Channel Ten na mtu mmoja amejeruhiwa aliyekuwemo ndani ya gari hiyo aliyefahamika kwa jina la Mziray Abedi, mkazi wa Lindi,"amesema RPC Mutayoba.

Josephine Kibiriti

Amesema kuwa miili ya marehemu hao imehifadhiwa kwenye Kituo cha afyà Ikwiriri pamoja na majeruhi huyo anaendelea kupata matibabu kwenye kituo hicho

Chanzo: www.tanzaniaweb.live