Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waajiri wasiopeleka michango ya wafanyakazi kubanwa

57a121f606a0f2f49dec86359694aa7f.jpeg Waajiri wasiopeleka michango ya wafanyakazi kubanwa

Sun, 2 May 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

SERIKALI imesema haitasita kuwachukulia hatua kali waajiri wote katika sekta za umma na binafsi ambao hawapeleki au kuchelewesha upelekaji wa makato ya wafanyakazi katika mifuko ya jamii ambayo wamejiunga nayo.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Aboubakar Kunenge alisema hayo jana kwenye sherehe za maadhimisho ya Siku Kuu ya Wafanyakazi ya Mei Mosi zilizofanyika katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam jana alipokuwa akihutubia wafanyakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Alisema serikali haiwezi kukaa kimya na kuangalia wananchi wake wakinyanyaswa na kudhalilishwa huku haki yao ya msingi ikichezewa.

Aliwashauri waajiri wote ndani ya jiji hilo kutekeleza sheria za mifuko ya jamii kikamilifu na kwa wakati ili kukwepa mikwaruzano na serikali.

Alisema mkoa wake hautawafumbia macho watendaji wa serikali ambao hawatekelezi wajibu wao na badala yake wanawaachia watu wengine kufanya kazi zao.

Kwa upande wao wafanyakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam katika risala yao kwa mgeni rasmi, walimweleza baadhi ya changamoto zinazowakabili kuwa ni kulipwa mishahara duni hali inayowafanya kuendelea kutaabika kutokana na ugumu wa maisha uliopo.

Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania Mkoa wa Dar es Salaam Aboubakar Rashid alisema kilio kingine cha wafanyakazi ni pamoja na kukosekana au kuchelewesha mikataba ya hali bora kwa wafanyakazi ambayo itawawezesha wafanyakazi kupata maslahi bora.

Chanzo: www.habarileo.co.tz