Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

WIZARA ya Kilimo imesema itajenga miundombinu ya skimu ya umwagiliaji

433a8fb3fc9761ad2d5b3ca6f5de3c76 WIZARA ya Kilimo imesema itajenga miundombinu ya skimu ya umwagiliaji

Tue, 20 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WIZARA ya Kilimo imesema itajenga miundombinu ya skimu ya umwagiliaji katika kata ya Imalilo Songwe wilaya ya Mbarali yenye eneo linalokadiriwa kuwa hekta 6,500 baada ya kukamilika kwa utekelezaji wa maagizo ya Rais John Magufuli kupitia kamati ya mawaziri.

Kauli hiyo ya serikali imetolewa mwishoni mwa wiki na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya wakati akizungumza na wakulima wa mpunga wa skimu ya umwagiliaji ya Nguvukazi Mwanavala wilayani Mbarali akiwa ziarani kukagua shughuli za kilimo.

Kusaya aliwataka wakulima wa skimu hiyo inayolimwa kwa kutumia miundombinu ya kienyeji takribani hekta 6,500 kati ya eneo lote linalofaa kwa umwagiliaji la hekta 9,500 toka mto Ruaha kijiji cha Songwe, Ibumila ambapo wakulima wamejenga banio la asili.

Akiwa kijijini hapo, Katibu Mkuu huyo alitembelea mashamba ya wakulima, kukagua mfereji mkuu uliochimbwa na wakulima wenye urefu wa kilometa nane na pia alitembelea Kiwanda cha kukoboa mpunga cha Ubaruku kinachoendeshwa na ushirika wa wakulima hao na kuahidi kutatua changamoto za upatikanaji soko la mchele.

Akijibu risala ya wakulima kuomba kupatiwa msaada wa kujengewa mtaro wa kisasa wa umwagiliaji, Kusaya aliwataka wawe na subira wakati kamati ya mawaziri ikiendelea kutekeleza agizo la Rais Magufuli kuhusu kurasimisha vijiji 975 vilivyopo ndani ya hifadhi ili vitambulike na kuwa maeneo ya kilimo na ufugaji.

“Wakulima kuweni na subira tumalize kutekeleza maagizo ya Rais Magufuli ikiwemo kutambua mipaka ya kijiji na hifadhi kisha nitawatuma wataalamu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kuja hapa Ubaruku kufanya upembuzi yakinifu ili tuijenge skimu hii kisasa na kuweza kuongeza tija ya uzalishaji mpunga” alisisitiza Kusaya.

Lengo la wizara ya kilimo ni kujenga miundombinu ya kisasa ya umwagiliaji kwenye mashamba ya wakulima Mwanavala ili maji yasipotee bure alisisitiza Kusaya na kuongeza kuwa watalaamu wa Tume ya Taifa ya umwagiliaji watahusika kufanyaka kazi hiyo baada ya maagizo ya Rais kutekelezwa.

Akitoa tarifa ya ushirika wa shamba la Nguvukazi Mwanavala, Katibu wa kikundi hicho Christopher Uhagile alisema ushirika huo ulianza mwaka 2002 na kuwa sasa wana wanachama 3,500 wanaolima mpunga katika mfereji licha ya miundombinu kutokuwa ya kisasa.

Akizungumzia changamoto za kubomolewa kwa banio la mfereji wa umwagiliaji mwaka 2018 na mwekezaji hali iliyoyasabisha mgogoro na wakulima lakini wanashukuru uamuzi wa Rais Magufuli kuagiza banio hilo kujengwa na wakulima waruhusiwe kutumia maji.

Naye mwakilishi wa wakulima, Chubi Mbayinjini wa kitongoji cha Mnazi alisema wanashukuru uamuzi wa Rais Magufuli kuondoa GN 28 hali inayowafanya waendelee na kilimo katika mashamba ya Mwanavala.

Alitoa wito kwa uongozi wa bonde la mto Ruaha ili waruhusu kibali cha kutumia maji hayo kunusuru mazao ya wakulima kipindi cha ukame na kuwezesha uzalishaji mpunga kuongezeka zaidi.

Mbayinjini alisema wamekuwa wakifuatilia kibali cha kutumia maji ya bonde la mto Rufiji tangu mwaka 2001 bila majibu toka kwa wahusika hali inayowakatisha tamaa wakulima kuzalisha zaidi mpunga.

Katibu Mkuu Kusaya kufuatia ziara yake kwenye mashamba hayo ya mpunga ya wakulima wadogo Mwanavala aliridhishwa na kazi wanayoifanya na kuahidi kushirikiana na makatibu wakuu wa Wizara za Viwanda na Biashara naile ya Maji ili wafanye utatuzi wa changamoto za masoko ya mchele na kibali cha utumiaji maji.

Chanzo: habarileo.co.tz