Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

WANAFUNZI WAJERUHIWA BAADA YA KUANGUKIWA NA DARI FORODHANI

Dyzajn Bez Nazvy 2019 07 18t102249.172.jpeg WANAFUNZI WAJERUHIWA BAADA YA KUANGUKIWA NA DARI FORODHANI

Wed, 11 Nov 2020 Chanzo: zanzibar24.co.tz

Wanafunzi wawili wa Shule ya Sekondari ya Forodhani iliyopo Mji Mkongwe Mkoa wa Mjini Magharib Unguja wamepata majeraha baada ya kuangukiwa na dari wakia umelala kambi skuli hapo kwa ajili ya maandalizi ya mitihani ya kidato cha pili na cha nne.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa huo Awadhi Juma Haji amsema tukio hilo limetokea mnamo tarehe 11-11-2020 majira ya saa 9:30 alfajir ya leo huko Shule ya Sekondari ya Forodhani .

Ameongeza kusema kuwa waliolala  sehemu ya varanda ambao ni wanafunzi wa kidato cha nne ambao wameagukiwa na dongo la dari na kusababisha kupata madhara.

Amewataja wanafunzi waliodhurika na dongo hilo akiwemo Abdulimajid Ameir  Silima mwenye umri wa miaka 17 mkaazi wa Mtoni Kidatu ambae ameumia mkono wa kulia ametibuwa hospitali ya mnazi mmoja na kuruhusiwa  na mwengine Mohammed  Suleiman Rashidi mwenye umri wa miaka 18 mkaazi wa mtoni kidatu ambae amepata madhara ya kuumia mwilini sehemu ya mbavuni na kichwani na anaendelea na matibabu katika hospitali ya mnazi mmoja.

Kamanda Awadhi amesema chanzo cha tukioni unyevunyevu wa kutuwama kwa maji juu ya dari hiyo pamoja na uchakavu wa dari ambao umepelekea plasta kubanduka na kuwaangukia wahanga hao.

Sambamba na hayo Kamanda Awadhi amewataka wahusika wa majenzi wa mji mkongwe na wahusika wengine kufanya marekebishwa katika majengo hayo ili kuepusha ajali ambazo zinaweza kuepukika .

Story na Rauhiya Mussa Shaaban.

Chanzo: zanzibar24.co.tz