Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vyumba vya madarasa mwiba kwa wakurugenzi

31860 Wanafunzipic TanzaniaWeb

Sat, 15 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Babati.  Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, Missaile Mussa amewaagiza wakurugenzi watendaji wa Halmashauri za mkoa huo, kuhakikisha wanafunzi wote 5,000 waliochaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari na kukosa nafasi, wanaanza kidato cha kwanza mwakani.

Mussa ameyasema hayo leo Desemba 15, 2018 mjini Babati, wakati wa kikao cha kamati  ya uchaguzi wa wanafunzi wa kuingia kidato cha kwanza mwaka, 2019.

Amesema ni haki ya wanafunzi hao kuingia kidato cha kwanza Januari au Februari mwakani kwakuwa wamechaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari.

“Hakikisheni wanafunzi wote waliochaguliwa kujinga na sekondari wanachaguliwa ili waweze kujiunga na sekondari na muda umebaki mdogo mno,”  amesema Mussa.

Ofisa Elimu wa mkoa wa Manyara, Anorld Msuya alisema wanafunzi 21,453 sawa na asilimia 70.79 yahoo waliofanya mtihani wa kuhitimu darasa la  saba walifaulu.

Msuya amesema wanafunzi 16,061 sawa na asilimia 74.87 ya waliofaulu watapata nafasi ya kuingia kidato cha kwanza mkoani humo.

Amesema kwa upande wa shule za kutwa zipo sekondari 137 ambapo zitachukua wanafunzi 19,950 wakiwemo wavulana 9,475 na wasichana 10,475.

Amesema kuna nafasi za shule za bweni zipo 105 na wanafunzi wengine watakwenda kwenye sekondari za Pugu, Malangali, Balangdalalu na Ifunda.

Mwanafunzi wa shule ya awali na msingi Amka Africa ya mjini Babati, John Petro ambaye alishika nafasi ya kwanza kimkoa amesema nidhamu na kusoma kwa bidii ndiyo siri ya mafanikio yake.

Petro amesema ataendelea kuwasikiliza walimu kwenye masomo yake ili atimize ndoto zake za kuwa mhandisi wa ujenzi kwenye miaka ya mbeleni.



Chanzo: mwananchi.co.tz