Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vyandarua havipunguzi nguvu za kiume

Chandarua Vyandarua havipunguzi nguvu za kiume

Fri, 29 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Wilaya ya Nzega Naitwapwaki Tukai, amesema hatomvumilia na atakula sahani moja na yeyote atakayehujumu vyandarua vya Serikali kwa kuuza au kufugia kuku kwa kisingizio kuwa vinapunguza nguvu za kiume “Kama hauna nguvu za kiume hauna tu”

“Nzega inahitaji Watu Waaminifu, sitavumilia Mtu atakayeuza vyandarua vya Serikali, Wafanyabiashara msijaribu nikikuta dukani kwako wewe ni Muhujumu, utalipa vile ninavyotaka Mimi au kufilisiwa hii ni mali ya Serikali, niwatake Wanawake wenzangu msikubali kudanganywa na kukimbiwa kitandani, Mwanaume hawezi kukosa nguvu kwa kulala katika neti yenye dawa kama hauna nguvu hauna tu”

DC Tukai amesema hayo Mkoani Tabora, katika usambazaji wa vyandarua unaofanywa na Bohari ya Dawa (MSD), ambapo amesema hatokubali kuona jitihada za Rais Dk. Samia Suluhu Hassan za kuboresha maisha ya Watanzania na Sekta ya Afya zinarudishwa nyuma kwa makusudi, hususani kwa kukwamisha mradi huo wa usambazaji wa vyandarua kwa Wananchi.

Mwananchi mmoja aitwaye Richard Sendela Mkazi wa Utemi, Nzega Mjini, amesema “Mimi natumia vyandarua hivi na nimeoa tangu mwaka 1970 nina Mke mmoja tumezaa Watoto tisa na nina Wajukuu 30 na nguvu bado ninazo hayo ni maneno ya uongo vijana wetu wale vizuri”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live