Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vurugu zaibuka mwenge wa uhuru ukizindua mradi

Vuruguu 3516995 Vurugu zaibuka mwenge wa uhuru ukizindua mradi

Fri, 5 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Mwenge wa uhuru ukikagua baadhi ya miradi Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro kumeibuka Vurugu katika eneo la mradi la Shirinjoro baada ya wananchi waliopo pembezoni mwa eneo hilo kuibuka na mabango wakidai kudhulumiwa

Vurugu hizo zimeibuka juzi Aprili 3, 2024 baada ya wananchi hao kunyang'anywa mabango yao na baadhi ya askari waliokuwepo eneo hilo, hali iliyozua taharuki kubwa.

Hata hivyo, Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa, Godfrey Mnzava aliingilia kati suala hilo na kumtaka mkuu wa wilaya hiyo, Amir Mkalipa pamoja na vyombo vyake vya usalama kuhakikisha wanasimamia sheria ya kuvilinda vyanzo vya maji.

Wakizungumzia eneo hilo, wananchi hao wamesema eneo hilo lilikuwa likitumiwa na mababu zao na yapo baadhi ya maeneo wamezika ndugu zao.

Lilian Chami, mkazi wa eneo hilo, amesema shamba hilo ni la urithi kutoka kwa babu yao na kwamba wataalamu wa bonde la mto Pangani walifika kuweka alama (bikoni) bila kuwashirikisha.

“Hili ni shamba la urithi la babu yetu Shirinjoro, nalalamikia uwekaji wa bikoni. Kwanza zimewekwa bila taarifa, nimekuja kuambiwa na wananchi na miti ikiwa tayari imepandwa.

"Pale walipopima mita 60 katika shamba langu imekula nusu ya shamba, lakini pia hizo mita 60 wamepima katika dimbwi la maji na si kwenye chanzo na watu wa Pangani wanasema kile ni chanzo cha maji," amesema na kuongeza;

"Ninachokiomba tumekuwa pale miaka na miaka, tumefuga na mbaya zaidi walishapitisha sheria na kuweka mawe kuonyesha mwisho wa barabara, naomba mama Samia (Rais Samia Suluhu Hassan) alitazama hili jambo kwa macho mawili, kwani mimi hapa sina shamba la kulima na sijui watoto wala wajukuu watakula nini... kama ni kuondoka waangalie tupate fidia."

Dativa Beda amesema, "walikuja wakapima wakaweka bikoni na kuotesha miti, wakasema watakuja kung'oa nyumbami hivyo tulhamie na walitupa siku 90."

Ally Mushi, amesema familia zilizopo eneo hilo ziliachwa mashamba hayo kwa ajili ya kuendeshea familia zao, hivyo kuhitajika mazungumzo kabla ya kuwekwa alama ili kuwezesha eneo hilo kulindwa kikamilifu.

"Wako wanaosema sisi tunaambiwa tuondoke na hatujalipwa fidia, lakini wanapokuja kuweka bikoni na kuwaruka wadau wenzao ambao ni wananchi, tujiulize msitu huo utaendelea kuwepo?" amehoji.

Akitoa maelekezo, kiongozi huyo wa mbio za mwenge, Godfrey Mnzava alimtaka mkuu wa wwilaya hiyo, Amir Mkalipa pamoja na vyombo vyake vya usalama kuhakikisha wanasimamia sheria ya kuvilinda vyanzo vya maji.

"Katika hilo hakuna namna yoyote kupindisha wala kulegalega, tunakupongeza kwa hatua ambazo mmeendelea kuchukua, tuna sheria namba 20 ya mwaka 2004, lakini pia imerejewa mwaka 2009 ambayo inaelekeza katika vyanzo vyote vya maji, mito, bahari, mabonde maziwa, chemchem na vyanzo vingine vya maji, shughuli zote za kibinadamu ndani ya mita 60 haziruhusiwi.

Mnzava amesema Mwenge wa Uhuru umeenda mahali hapo mahususi na hakuna kufanya shughuli zozote za kilimo na za kibinadamu ndani ya mita 60 kutoka kwenye vyanzo vya maji huo, ndio msimamo wa Serikali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live