Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viwanda 148 vyaanzishwa Iringa

Ab704959ead5fab61f6134d722a4418c Viwanda 148 vyaanzishwa Iringa

Mon, 25 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

JUMLA ya viwanda 148 vimeanzishwa mkoani Iringa kuanzia mwaka 2015 ambapo kati ya viwanda hivyo viwanda 138 ni vidogo na viwanda saba ni vya kati na viwanda vitatu ni vikubwa.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi, wakati akitoa taarifa ya uwekezaji mkoani humo mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ambaye leo anazindua Mwongozo wa Uwekezaji mkoani humo.

Hapi amesema mafanikio hayo ni matokeo ya hatua mbali mbali za makusudi ambazo Mkoa huo umechukua ikiwa ni pamoja na kuanzishwa kwa kitengo maalum ambacho kimekuwa kikihudumia wawekezaji mbali mbali.

Amesema kitengo hicho tangu kuanzishwa kwake tayari kimehudumia wawekezaji wakubwa 50 kwa kuwasaidia kupata ardhi kwa wakati, kutatua migogoro, kusaidia upatikanaji wa vibali na kuwasiliana na taasisi mbali mbali za seriklai lengo likiwa ni kuchochea uwekezaji.

Aidha Hapi amemuahidi Waziri Mkuu kuwa mbali na kuvutia wawekezaji, Mkoa wa Iringa utaendelea kuwahudumia kwa karibu wawekezaji ambao tayari imewapata ili wawe mabalozi wa kuvutia wawekezaji wengine.

Chanzo: habarileo.co.tz