Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vivuko Kigongo/Busisi kuhamishwa

Busisi (600 X 338) Vivuko Kigongo/Busisi kuhamishwa

Wed, 17 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, imewaagiza wakala wa huduma za Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA), kufanya tafiti za masoko katika ziwa Victoria, ili kuviwezesha vivuko vya Kigongo/Busisi mkoani Mwanza, kuendelea kutoa huduma baada ya daraja la JPM kukamilika.

Ujenzi wa daraja la (JPM) lililopo eneo la Kigongo/Busisi, umefikia zaidi ya asilimia 31%, hatua inayoilazimu Wizara hiyo kuwaagiza wakala hao, kufanya tathmini ya kuvitafutia maeneo ya kutoa huduma vivuko hivyo, baada ya daraja hilo kukamilika ifikapo April mwaka 2024.

Aidha Wizara imesisitiza kufanyika haraka kwa tathimini hizo ili kufanikisha suala la usarifi katika maeneo hayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live