Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vitongoji 286 kupata umeme wa REA

Mgao Umeme.jpeg Vitongoji 286 kupata umeme wa REA

Fri, 3 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MRADI wa Ujazilizi wa Kusambaza Umeme vijijini kwenye maeneo yaliyokosa nchini umeanza kutekelezwa na utanufaisha vitongoji 286 vya Mkoa wa Morogoro.

Wananchi wa Malinyi mkoani Morogoro wameelezwa hayo mbele ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Daniel Chongolo aliye ziarani mkoani humo kukagua miradi ya maendeleo na kuzungumza na wanachana wa CCM na wananchi.

Akijibu kero ya ukosefu wa umeme kwenye baadhi ya vitongoji wilayani Malinyi,Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), mkoani Morogoro,Fadhili Chilombe amesema ni kweli baadhi ya vitongoji katika vijiji mmkoani humo havijafikiwa na nishati hiyo.

Katika miradi inayotekelezwa sasa ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kuna vitongoji vimeachwa na sasa vitanufaika katika mradi huo mpya ulianza kutekelezwa Februari Mosi.mwaka huu.

Katika mradi huo ,Mkoa wa Morogoro jumla ya vitongoji 286 ,vinanufaika na mradi huo wa ujazilizi na vitongoji vya Wilaya ya Malinyi navyo vitanufaika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live