Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vitongoji 208 kufikishiwa umeme kabla ya 2025 Sengerema

Umeme 1 Vitongoji 208 kufikishiwa umeme kabla ya 2025 Sengerema

Sun, 19 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Sengerema. Vitongoji 208 kati ya 412 vilivyopo Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza vinatarajiwa kufikishiwa huduma ya umeme kabla ya mwaka 2025.

Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) wilayani Sengerema, Martin Kilenga ameliambia Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Sengerema kuwa hadi sasa tayari vitongoji 213 vimefikishiwa nishati hiyo.

Amesema Tanesco imekuja na mpango mkakati mpya ambao umelenga kuhakisha kabla ya mwaka 2025 vitongiji hivyo ambavyo havijafikiwa na huduma ya umeme viwe vimefikiwa.

"Ninawahakikishia Tanesco tuko vizuri kuhakikisha miradi yote inakamilika...kabla ya mwaka 2025 Vitongoji vyote vitakuwa vimepata umeme,”amesema Kalenga

Hoja ya Vitongoji hivyo kupata umeme iliwasilishwa na Diwani wa Kata ya Katunguru, Saidi Jimola aliyewaomba Tanesco kuhakikisha wanapeleka umeme kwenye vitongiji vyote ikiwemo Juma kisiwa ambako hakuna umeme.

Kauli hiyo iliungwa mkono na baraza hilo akiwemo diwani wa Kata Tabaruka, Sospeter Busumabu kutokana na wananchi wa vitongoji hivyo kuhangaika kutokana na ukosefu wa huduma hiyo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Sengerema, Yanga Makaga amepongeza mkakati wa Tanesco kuwahakikishia wananchi kuwa kabla ya mwaka 2025 umeme utakuwa umeenea kwenye vitongiji vyote.

Yanga amezitaka taasisi zingine wilayani humo kuiga mfanao wa Tanesco kuwasilisha taarifa zao na kuzitolea ufafanuzi kisha kupata ufumbuzi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live