Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viti 50 vya watu wenye ulemavu vyatolewa Mara, Simiyu

65207 Pic+viti

Tue, 2 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti. Kampuni ya Utalii ya Tanzania Trucker Safaris (TGT) inayofanya biashara Wilaya za Maswa Mkoa wa Simiyu na Serengeti mkoani Mara imetoa viti 50 kwa watu wenye ulemavu vyenye thamani ya zaidi ya Sh20 milioni.

Meneja wa kambi ya utalii ya kampuni hiyo Suli Ngeya leo Jumanne Julai 2,2019 akitoa ufafanuzi wa msaada huo uliokabidhiwa kwa Mbunge wa Serengeti (CCM) Marwa Ryoba amesema wamekuwa wakitoa misaada mingine ya kijamii lakini sasa wameamua kujielekeza kwenye makundi maalum ambayo yamesahaulika.

Naye Ryoba amesema msaada huo ni mkombozi kwa wahitaji wengi kwa kuwa wengi hawakuwa na uwezo wa kulipia zaidi ya Sh400,000 kwa kiti kimoja.

Kwa upande wake, Hamisi Shabuke mmoja wa wanufaika amesema watu wenye ulemavu wamekuwa wakisahaulika kwenye misaada mbalimbali na kupongeza utaratibu wa kampuni hiyo unatakiwa kuigwa na kampuni mengine.

Chanzo: mwananchi.co.tz