Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vitambulisho 15,000 vya wajasiriamali vyakabidhiwa Mwanza

VITA.webp Vitambulisho 15,000 vya wajasiriamali vyakabidhiwa Mwanza

Wed, 20 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakuu wa Wilaya zote Mkoa wa Mwanza na Wakurugenzi wa Halmashauri mkoani humo wamekabidhiwa vitambulisho 15,000 vya Wafanyabiashara wadogowadogo (Machinga ) vyenye thamani ya million 300.

Akizungumza wakati akikabidhi vitambulisho hivyo kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amesema vitambulisho ambavyo vinapaswa kupokelewa mkoani humo ni 88,000 vyenye thamani ya billion 1.76, ambapo awamu ya kwanza wamepokea vitambulisho 15,000. Amesema wanategemea katikati ya mwezi ujao Juni mwaka huu watakabidhiwa vitambulisho 73,000 vilivyobaki ili ikifika Disemba mwaka huu wawe wamemaliza kuuza vitambulisho vyote 88,000. Amesema kuwa kwa utendaji wa viongozi hao wa kufanyakazi ana imani katika hilo ufanisi, utakuwa juu katika kutekeleza maelekezo ya Rais katika kundi hilo lenye vijana na wanawake wengi ambao ni wajasiriamali ambalo ni kundi muhimu katika uchumi wa nchi.

Mongella amewataka viongozi hao kuwa waadilifu na waaminifu sambamba na kuchapa kazi katika kusambaza vitambulisho hivyo kama walivyosimamia miradi ya maendeleo kwani Rais ameifanya hivyo kwa ajili ya kuondoa adha na usumbufu kwa wafanyabiashara hao. "Tulijifunza mengi kwa zoezi lililopita tutumie uzoefu tuliopata kufanya marekebisho na kufanya zoezi hili liwe na ufanisi zaidi bila ya kuwa na kero kwa mtu yoyote na wasijihisi kuwa mzigo wao pekee bali ni wa wote hivyo kikubwa ni ushirikianao ambao utasaidia kusogeza maendeleo mbele na kufanikisha jambo hili,"amesema Mongella.

Sanjari na hayo ametumia fursa hiyo kuwataka viongozi hao katika kipindi cha robo ya mwisho wa mwaka kuzingatia ukusanyaji wa mapato ili kufikia malengo yao walioyaweka pamoja maelekezo na kufikia asilimia 100. Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza, Emmanuel Tutuba, amesema vitambulisho hivyo wamevipokea kutoka kwa Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Mwanza na vimegawiwa katika Halmashauri nane na Wilaya saba za mkoa huo ikiwemo Halmashauri ya Jiji la Mwanza ambao wamepokea vitambulisho 3,500,Ilemela 3,000,Sengerema 1,500,Buchosa 1,500,Ukerewe 1,000,Kwimba 1,500,Misungwi 1,500 na Magu 1,500 ambapo zoezi hilo limefanyika huku wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wakishuhudia. Naye Meneja wa TRA Mkoa wa Mwanza, Joseph Mtandika amesema mwaka jana walipokea vitambulisho 80,000 ambapo walivigawa vyema jambo lililochochea mwaka huu kuongezewa idadi huku vitambulisho vya mwaka huu vina serial namba hivyo wafanyabiashara wavitendee haki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live