Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vitabu vinavyohamasisha Mapenzi ya Jinsia moja vyakamatwa Tabora (+Video)

Vlcsnap 2024 05 21 21h19m48s036 1024x576.png Vitabu vinavyohamasisha Mapenzi ya Jinsia moja vyakamatwa Tabora

Tue, 4 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali Mkoa wa Tabora imekamata shehena ya vitabu vyenye machapisho ya kufundisha na kuhamasisha vitendo vya mapenzi ya jinsia moja kwa wanaume na wanawake ambavyo vilikuwa mbioni kuanza kusambazwa katika shule za msingi na sekondari Wilayani Kaliua kupitia Taasisi isiyo ya kiserikali ya Athumani Kapuya

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Paulo Chacha akiwa katika Wilaya ya Kaliua amesema vitabu hivyo vimewekwa kizuzini baada ya serikali kupitia watalamu wake kubaini kuwepo kwa uchafu wa maudhui katika vitabu hivyo ambayo vimeingizwa Wilayani humo na Taasisi isiyo ya kiserikali ya Athumani Kapuya kwa lengo la kuvitoa msaada kwa shule za msingi na sekondari.

Akizungumza Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Dkt . Amini Joseph ameongeza kuwa Msaada huo wa vitabu uliingizwa Sanjali na vifaa tiba ikiwemo vilainishi na taulo za kike.

Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Dkt. Rashidi Chua chua amesema shehena hiyo imekamatwa ikiwa na vitabu zaidi ya elfu nane ambavyo huenda vingezifikia shule za msingi 139 na za sekondari 32 katika wilaya hiyo.

Kufuatia Sakata hilo Mkuu wa Mkoa wa Tabora Paul Chacha ameifungia Taasisi hiyo isiyo ya kiserikali ya Athumani Kapuya kutokuendesha shughuli zake ndani ya Mkoa wa Tabora wakati huo akiagiza kukamatwa kwa waratibu na viongozi wa Taasisi hiyo

View this post on Instagram

A post shared by Wasafi FM (@wasafifm)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live