Viongozi wa Halmashauri ya Mbinga Mji Mkoa wa Ruvuma wamepewa siku saba kurejesha trekta la halmashauri lililouzwa kinyume cha utaratibu na idara ya manunuzi ya halmashauri hiyo.
Viongozi wa Halmashauri ya Mbinga Mji Mkoa wa Ruvuma wamepewa siku saba kurejesha trekta la halmashauri lililouzwa kinyume cha utaratibu na idara ya manunuzi ya halmashauri hiyo. Kupitia baraza la madiwani linaloendelea muda huu, Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Aziza Mangosongo amemwagiza Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Kelvin Mapunda kurejesha trekta hilo pamoja na tela lake ili mnada ufanyike upya kwa utaratibu unaotambulika.