Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viongozi wamiminika Morogoro, mkuu wa mkoa asema vifo walioungua na mafuta vyafikia 68

70876 Pic+viongozi

Mon, 12 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Morogoro/Dar. Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameungana na viongozi wengine wa vyama na Serikali mkoani Morogoro kwenye msiba wa kitaifa baada ya kutokea ajali ya moto iliyoua Watanzania 68 hadi leo Jumapili Agosti 11, 2019 saa 3 asubuhi.

Kwa mujibu wa mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Stephen Kebwe amesema idadi hiyo imeongezeka kutoka vifo 64 vilivyoripotiwa hadi jana saa 10 jioni hadi vifo 68.

Ajali hiyo ilitokea jana Jumamosi Agosti 10, 2019 katika kijiji cha Itigi, Msamvu mkoani Morogoro   baada ya lori la mafuta kupinduka na kuwaka moto muda mfupi baada ya watu kuanza kuchota mafuta.

Picha za video zinaonyesha lori hilo likiwa limepinduka barabarani na mafuta yakichuruzika kuelekea pembeni mwa barabara ya Morogoro- Dar es Salaam ambako watu waliokuwa na madumu ya ujazo mbalimbali walikuwa wakichota mafuta kabla ya moto kuwaka.

Mbali na Majaliwa, viongozi wengine waliomiminika mkoani humo ni Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu,Sera, Bunge,Ajira, Kazi,Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama; Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe; mganga mkuu wa Serikali ya Tanzania, Profesa Mohamed Kambi.

Katibu mkuu Wizara ya Afya, Dk Zainabu Chaula; katibu mkuu Wizara ya Mambo ya Nje, Meja Jenerali Jacob Kingu; kamishna wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengeye; mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Dk Dk Modestus Kipilimba; Kamanda wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Fortunatus Muslimu; naibu Waziri wa Kilimo, Omary Mgumba na Waziri wa Tamisemi, Seleman Jafo.

Habari zinazohusiana na hii

Naye mkuu wa kitengo cha mawasiliano Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Aminiel Aligaesha amesema hospitali hiyo imeshapokea majeruhi 30 wa ajali ya hiyo.

Aligaesha amesema timu ya wataalamu kutoka Muhimbili ilifika mkoani Morogoro na kubaini kati ya majeruhi 70,  47 wanatakiwa kufikishwa katika hospitali hiyo.

Amesema majeruhi wengine watawasili Muhimbili leo wakitokea Morogoro baada ya mapema leo kuwasili 30 kati ya 47.

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi

Chanzo: mwananchi.co.tz