Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viongozi wa vyama vya ulemavu wapewa somo

72871251059f6d88770434ff96230008 Viongozi wa vyama vya ulemavu wapewa somo

Mon, 30 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

SERIKALI imewataka viongozi wa vyama vyote vya watu wenye ulemavu nchini kutengeneza mazingira mazuri ya kuwakutanisha watu wenye ulemavu hatua itakayowezesha kujiunga katika vikundi mbalimbali vitakavyowezesha kupewa mikopo.

Aidha alizitaka taasisi mbalimbali za binafsi na serikali nchini kushirikiana na taasisi ya Regnald Foundation (DRMF) katika kuzikabili changamoto mbalimbali zinazowakabili watu wenye ulemavu nchini.

Akizungumza kwa niaba ya serikali wakati wa hafla ya watu wenye ulemavu iliyotanguliwa na matembezi ya hisani ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Ng'wilabuzu Ludigija alisema kuna kila sababu ya walemavu hao kupata fursa ya mikopo mbalimbali inayotolewa na serikali hivyo ni vyema wakapewa elimu ili kuunda vikundi vyao.

Alisema mara nyingi jamii ya watu wenye ulemavu nchini imekuwa ikikabiliwa na changamoto nyingi ambazo pasina kuwa na vipato vya kuzitatua kuawaweka katika wakati mgumu wa kuendesha maisha yao na kwamba fursa pekee ya wao kuitumia ni mikopo inayotolewa na serikali kupitia halmashauri mbalimbali.

"Serikali imekuwa ikijali na kuwajali watu wenye ulemavu mbali na fursa zingine inazotoa kwao pia imeweka utaratibu mzuri wa kuwapa mikopo isipokuwa changamoto iliyojitokeza kwao ni kutojiunga katika vikundi kama kigezo cha kupewa mikopo hiyo," alisema Ludigija.

Alisema katika halmashauri za jiji la Dar es Salaam, Wilaya ya Ilala inaongoza kwa kutoa mikopo kwa watu wenye ulemavu ambapo kwa kipindi cha mwaka jana pekee wameweza kutoa kiasi cha zaidi ya Sh bilioni 2 kwa vikundi vya watu wenye ulemavu.

Alivitaka vyama mbalimbali vya watu wenye ulemavu kuhakikisha wanakuwa karibu nao na kuwapa elimu ya kutosha ili waweze kujiunga na vikundi hivyo kwa ajili ya kupewa mikopo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Shiminana Ntuyabaliwe taasisi ya Regnald Foundation wakati siku ya watu wenye ulemavu kitaifa ikitarajiwa kuadhimishwa Desemba 3 jijini Dodoma ,taasisi hiyo iliona bora kuwakutanisha pamoja walemavu hao sambamba na kufanya matembezi ya hisani kwa ajili ya kuchangisha fedha zitakazosaidia matibabu kwa wenye matatizo mbalimbali ya kiafya.

Alisema kwa mwaka huu, taasisi hiyo imelenga kuwezesha matibabu kwa walemavu wenye matatizo ya utoaji, ugonjwa wa akili pamoja na ugonjwa wa saikolojia ambayo kwa pamoja hujulikana kama magonjwa yasiyotambulika

Aidha alipongeza serikali chini ya Rais John Magufuli kwa kuonyesha kwa vitendo kuwajali watu wenye ulemavu ikichukua hatua mbalimbali kushughulikia changamoto zinazowapata suala aliosema linaipa faraja kubwa taasisi hiyo aliyoanzishwa na hayati Regnald Mengi

Alisema kupitia mabalozi mbalimbali wakiwemo wabunge wanaowakilisha makundi ya watu wenye ulemavu na wengine kunipa hamasa taasisi hiyo kushughulikia kero mbalimbali za watu wenye ulamavu .

Chanzo: habarileo.co.tz