Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viongozi 52 kati ya 120 wa vyama vya ushirika Maswa wakamatwa

29529 Pic+viongozi TanzaniaWeb

Fri, 30 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Maswa. Viongozi wa Vyama vya Msingi Vya Ushirika (Amcos) 52 kati ya 120  wa Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu wamekamatwa na polisi wilayani humo.

Kukamatwa kwa viongozi hao kunatokana na agizo la Mkuu wa Wilaya hiyo, Dk Seif Shekalaghe baada ya kudaiwa kutumia fedha za kampuni za kununua na kuchambua Pamba mkoani Simiyu kukopeshana na kushindwa kuzirejesha huku wengine wakitokomea kusikojulikana.

Viongozi hao walijikutana mikononi polisi baada ya kumalizika kwa mkutano uliyoshirikisha Amcos zote za wilaya na kuhudhuriwa na wajumbe 400.

Dk Shekalage alitoa agizo la kukamatwa kwa viongozi wa bodi za Amcos hizo pamoja na viongozi wakuu wao.

Amesema hatua hizo zimechukuliwa baada ya kufanyika kwa uhakiki wa awali ambao bado unaendelea kufanyika na  kubaini Sh242 milioni ndizo zinapaswa kurejeshwa kwa kampuni za kununua pamba na siyo Sh272 milioni kama baadhi ya Amcos zilivyokuwa zikieleza hapo awali.

Amesema kampuni za kuchambua pamba ziliwazosilisha madai yao kwa uongozi wa wilaya hiyo zinadai Sh 461 milioni kutoka kwa Amcos za wilaya hiyo, lakini baada ya viongozi kufanya uhakiki wa awali ulibaini kampuni hizo zinadai Sh317 milioni tu.

“Kwenye Amcos tumebaini madeni yanayotakiwa kulipa kwa kampuni hizo ni  Sh242 milioni na sio Sh272 milioni kama zilivyowasilisha.”

“Hapa tumebaini kuna kama Sh30 milioni na kitu hazipo. Uchunguzi umebaini viongozi hawa walikopeshana hizi fedha na kushindwa kuzirejesha. Leo nataka fedha uuze ng’ombe au la! ninachotaka ni fedha,” amesema Dk Shekalaghe.

Dk Shekalaghe amesema hatua hiyo ni ya awali na kwamba uhakiki bado unaendelea na hatua zaidi zitaendelea kuchukuliwa kwa viongozi wa Amcos ambao wametafuna fedha za kampuni za kununua pamba wilayani humo na kuharibu utaratibu mzima wa Serikali kurejesha vyama vya msingi vya ushirika.

Katika hatua nyingine Dk Shekalage aliagiza kusimamishwa kazi kwa ofisa ushirika wa wilaya hiyo, Gorge Budodi kwa madai ya kutotimiza wajibu wake na kuacha majukumu anayopaswa kufanya yafanywe na mkuu wa wilaya hiyo.



Chanzo: mwananchi.co.tz