Wakazi wa vijiji vinne vya Tarafa ya Masasi wilayani Ludewa mkoani Njombe vinaenda kuondokana na changamoto ya kuhatarisha maisha yao kwa kuliwa na Mamba pindi waendapo kuchota maji katika mto Ruhuhu baada ya serikali kupeleka mitambo ambayo tayari imekwishaanza kuwachimbia visima na vitakavyowapatia maji safi na salama.
Wakazi wa vijiji vinne vya Tarafa ya Masasi wilayani Ludewa mkoani Njombe vinaenda kuondokana na changamoto ya kuhatarisha maisha yao kwa kuliwa na Mamba pindi waendapo kuchota maji katika mto Ruhuhu baada ya serikali kupeleka mitambo ambayo tayari imekwishaanza kuwachimbia visima na vitakavyowapatia maji safi na salama. Hatua hiyo imefikiwa mara baada ya wananchi hao kufikisha kilio chao kupitia vyombo vya habati pamoja na mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga ambaye hivi karibuni alishindwa kuendelea na mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kiyogo kilichopo katika kata ya Masasi kutokana na wananchi hao kuimba nyimbo za huzuni juu ya kukosa huduma ya maji huku wakibubujikwa na machozi kitu ambacho kilimlazimu mbunge huyo kuahirisha mkutano na kuahidi kurejea tena pindi atakapopata maji hatimaye mbunge huyo amerejea tena kufanya mkutano huo akiwa na mitambo ya kuchimba visima hivyo.